Jumatatu. 29 Aprili. 2024

Tafakari

Jumatano, Mei 17, 2017

Jumatano, Mei 17, 2017.
Juma la 5 la Pasaka

Mdo 15:1-6;
Zab 122:1-5 (R. 1);
Yn 15:1-8.


KUONDOA MAJIVUNO NA UBINAFSI!

Kupunguza matawi ni muhimu kwa mti kama unapenda uzae mataunda mazuri au maua mazuri. Kama, kwa mfano, mti wa maua ya waridi unakuwa bila kupunguzwa, unatoa vimaua vidogo vingi, amabavyo ni dhaifu. Lakini kwa mti mzuri ulio pruniwa unatoa maua mazuri yenye afya. Yesu anatumia mfano kama huu kutufundisha somo kama hilo katika kuzaa matunda mazuri kwa ufalme wake. Anataka maisha yetu yawe yenye matunda mema na anataka kututumia sisi kama vyombo vyake vyenye nguvu ulimwenguni. Lakini tusipo ingia katika maisha ya kiroho ya kujipruni mara kwa mara , hatutakuwa vyombo ambavyo Mungu anaweza kuvitumia.

Kujipruni kiroho unachukua ile hali ya kumruhusu Mungu aondoe maovu katika maisha yetu ili fadhila ziweze kungaa. Na hili lina fanikiwa hasa tunapo mruhusu atupe unyenyekevu na kutuondoa katika maringo yetu. Hili linaweza kuumiza, lakini maumivu yanayo tokana na kunyenyekeshwa na Mungu ni ufunguo wa kukuwa kiroho. Kwa kukuwa katika unyenyekevu, tunakuwa zaidi katika kujikita katika chanzo chetu kuliko katika kukuwa katika hali zetu wenyewe, mawazo yetu wenyewe na mipango yetu wenyewe. Mungu katika hali ya juu kabisa ana hekima kuliko sisi na kama tutaendelea kumwelekea kila mara kama chanzo chetu, tutakuwa wenye nguvu zaidi na kujiandaa yeye afanye mambo makubwa zaidi kwa njia yetu.

Kujiruhusu kupruniwa kiroho maana yake ni kuachia yaondoke mapenzi yetu wenyewe na mawazo yetu. Maana yake tunaachia kujitawala wenyewe na kumwachia aliye mkuu wa kukuza akuze na kuchukua nafasi. Ina maana tuna mwamini yeye zaidi kuliko tunavyo jiamini sisi wenyewe. Hili linahitaji kufa kwa nafsi zetu wenyewe na unyenyekevu wa kweli na kukiri kabisa kwamba Mungu ndiye tegemeo letu kwa kila kitu, kama tawi linavyo tegemea mti. Bila mti, tutaseka na kufa. Mwamini yeye na mipango yake na tambua kuwa hii ndio njia pekee ya kuzaa matunda mema, ambayo Mungu anayataka kupitia wewe.

Sala: Bwana, ninakuomba upruni majivuno yangu na kuyatupa mbali na pia uovu wangu. Nitakase mimi kutoka katika dhambi zangu nyingi ili niweze kujikabidhi kwako kwa kila kitu. Na ninapo jifunza kujikabidhi kwako, ninakuomba uanza kuzaa matunda mema katika maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni