Alhamisi. 19 Septemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Agosti 01, 2016

Jumatatu, Agosti 1, 2016,
Juma la 18 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Alfonsi Ligori, Askofu na Mwalimu wa Kanisa.

Yer: 28:1-17;
Zab: 118: 29, 43, 79-80, 95, 102;
Mt: 14:13-21


KUMUONA MUNGU KATIKA NYAKATI NGUMU!

Leo tunasikia kuhusu Yesu kwenda sehemu ya faragha peke yake, na pia kuhusu muujiza wa wakuwalisha watu. Sehemu hii inatupeleka mbali kidogo kutoka kwenye tukio la kukatawa kicha kwa Yohane Mbatizaji na Herode. Hatuna uhukakika Yesu alijisikiaje kwasababu ya uhusiano uliokuwepo kati yake na Yohane Mbatizaji, lakini ukweli tunaoona ni kwamba Yesu ‘alihitaji kuwa peke yake mahali’. Yesu anahitaji kuwa mahali pake yake si kujificha ila alihitaji kutafakari kuhusu huzuni yake na pia kupata nguvu wakati wa majaribu. Kuwa mahali petu wenyewe wakati mwingine, sehemu ya pekee binafsi wakati mwingine ni jambo tunalohitaji kufanya pia kwaajili ya Imani yetu, katika maisha kwa ujumla na hata wakati tukiwa na magumu katika hali ya pekee. Ni sehemu ambayo tunaweza kwenda na kulia, kutoa yaliyo ndani, kuingia ndani kabisa, na kutafuta majibu ya maswali yetu. Kupata majibu ya maswali haitoshi tu kuwa sehemu pekee mwenyewe, inapaswa kuwa sehemu ambayo unakutana na Mungu, sehemu ambayo unahisi uwepo wa Mungu.

Wakati ukiwa na Mungu unaweza usitambue bali utatambua hitaji muhimu kwa mwanadamu. Katika hali ya nnjee inaweza kuonekana muujiza wa kujilisha lakini katika uhalisia ni kujilisha ndani ya moyo kwakukutana na Mungu. “na wote walikula na kusaza”. Njaa ya mwili na roho zote zilishibishwa.

Yesu-Mungu duniani, anaona mahitaji yao na kusikia kilio chao. Anatoa uponyaji na matumaini na anawalisha kila mmoja kwa mkate na samaki. Hakuna aliyeondoka akiwa hajatosheka. Kuna mengine mengi yaliobaki kwa wale wahitaji, “wakakusanya vikapaku kumi na viwili vilivyojaa vipande vilivyobaki”. Hili linawezekana tuu kati wanadamu kushirikiana. Mungu haitaji mambo mengi yawepo. Mungu yupo kila mahali katika vitu vidogo. Mungu anapatikana katika hali ya ujangwa wetu, pale ambapo hatuwezi kujitegemea wenyewe, tunapaswa kumuamini. Mungu yupo kila wakati tunapo jitahidi kumtafuta tukiwa katika hali ya upweke wetu. Upendo wa Mungu ulionekana msalabani, sehemu ya jangwa kabisa kupita yote. Je, nahisi nimepotea? Je najisikia nimeumizwa? Je mimi ni mpweke? Je, nipo jangwani natafuta majibu?

Sala: Ee Bwana, uje kunisaidia na uje unisaide hima. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni