Jumanne. 21 Mei. 2024

Tafakari

Jumatano, Juni 22, 2016

Jumatano, Juni, 22, 2016,
Juma la 12 la Mwaka wa Kanisa


2 Fal 22: 8-13, 23: 1-3;
Zab 118: 33-37, 40;
Mt 7: 15-20


FANYA UCHAGUZI WA HEKIMA ILI UWEZE KULETA MATUNDA MEMA!

Yesu alisema “utautambua mti kwa matunda yake.” Alitambua kuwa mti mzuri unazaa matunda mazuri na mti mbaya unazaa matunda mabaya. Wakati tunanunua matunda sokoni hasa machungwa kutaka kutambua kweli kama ni mazuri ni pale unapo onja moja, na sio kwa kutazama tuu rangi yake kwa macho. Wakati mwingine tunajishughulisha na jinsi tutakovyo onekana mbele za watu kwa kuvaa vizuri na kuwa safi, hii ni sawa lakini ukweli ni kwamba utendaji wa mtu ndio ukweli wa jinsi ya mtu alivyo sio mavazi. Tunaweza kuwadanganya wengi kwa muonekano wetu wa nje, lakini kudanganya huku huwa hakudumu kwa muda mrefu. Leo Yesu anatualika tujiulize: hivi mimi ninatoa matunda gani? Na anatuambia matunda yetu yanaweza kuwa mazuri tuu kwanjia ya maisha ya sala (kokomaa), sadaka (kupruni) na kuto fungamana na dhambi (kuweka dawa) na mali au malimwengu.

Sala: Bwana, matunda yangu yote sio mazuri sana. Nahitaji kurutubisha, maji, kukua na kupruni. Nipe hekima yako na mwangaza niweze kuchagua marafiki. Nisaidie niweze kukatilia mbali, kudhania vibaya wengine au kuwa na mtazamo mbaya katika maisha yangu.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni