Jumatano. 15 Mei. 2024

Tafakari

Jumatatu, Mei 15, 2017

Jumatatu, Mei 15, 2017.
Juma la 5 la Pasaka

Mdo 14:5-18;
Zab 115:1-4,15-16 (K. 1);
Yn 14:21-26.


MUNGU ANAISHI NDANI MWETU!

Watoto huwa wanaelewa kwamba Mungu anaishi ndani ya mioyo yao. lakini, kama ukiwauliza wamejuaje, utaona wanakutazama kama kuchanganyikiwa katika kujibu. Licha ya hayo, wao wanatambua kwamba Mungu anaishi ndani yao. Pengine wewe utajibu nini katika swali hili kwamba, “umejuaje Mungu anaishi ndani mwako?” Pengine unaweza kujikuta ukipotea katika kuelezea hali hii ya juu ya fumbo la Imani yetu. Tunatambua kwamba Mungu anapenda kushikilia mioyo yetu, kuongea na sisi, kutuimarisha, kutuongoza na kutulinda sisi. Tunatambua kwa zawadi ya Imani yetu, kwamba Mungu yupo na anatamani muunganiko wa ndani na sisi. Tunatamua tu hilo.

Imani inatuongoza kwenye uelewa, na kila mara tunapo isikiliza sauti ya Mungu inayo ongea ndani mwetu, ikituongoza na kutulinda sisi, ni mwanzo wa kuanza kuelewa kuishi kwake ndani mwetu. Kama Mt. Agustino anavyosema, “Imani ni kuamini kile usicho kiona. Na matokeo ya imani ni kuona kile unacho kiamini”. Imani kwa uwepo wa Mungu inatuongoza kwenye jibu la swali hapo juu. Nitafahamuje, Mungu anaishi ndani mwangu? Jibu ni kwamba ni kwasababu namuona ndani yangu, naongea na yeye ndani, na anaongea na mimi ndani. Na pia naona matokeo ya Imani yangu kwake kutokana na kuamini huku.

Muache yeye aongee na wewe, katika maongezi ya ndani, ruhusu kuishi kwake ndani kukuwe na kuthihirika kwa wengine. Mungu hapendi tu kuthihirika ndani mwako lakini pia anataka kungara kupitia wewe.

Sala: Bwana, njoo uishi moyoni mwangu. Fanya moyo wangu sehemu yako ya kuishi. Nisaidie niweze kukuona wewe hapo na kuongea na wewe na kukupenda wewe ndani ya roho yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni