Jumatano. 15 Mei. 2024

Tafakari

Jumapili, Mei 14, 2017

Jumapili, Mei 14, 2017.
Juma la 5 la Pasaka

Mdo 6: 1-7;
Zab 32: 1-5, 18-19;
1 Pet 2: 4-9;
Yn 14: 1-12.


MIMI NI NJIA, UKWELI NA UZIMA.

Je umekombolewa? “ndio” tumekombolewa kwa njia tatu: tumekombolewa kwa njia ya neema ya Ubatizo, tunaendelea kukombolewa kwa njia ya neema za Mungu na huruma tunapo amua kumfuata kwa uhuru kamili, na tunatumaini kokombolewa na kuingia katika utukufu wa Mbinguni.

Imekuwaje tumepokea zawadi ya thamani ya ukombozi? Kwa njia ya maisha, mateso kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ambaye ndiye pekee aliye njia ya kwenda kwa Baba. Njia pekee ya Ukombozi ni Yesu. Hivyo Yesu Kristo anapaswa kuwa kiini cha maisha yetu, na tunapaswa kumuona kama njia, ukweli na uzima. Yeye ni njia pekee ya Mbinguni, yeye ni utimilifu wa ukweli wote ambao tunapaswa kuuamini, na yeye ni uzima ambao tunapaswa kuuishi na yeye ndiye chanzo cha maisha mapya ya neema. Bila yeye sisi si kitu, bali kwa njia yake unapata maisha makamilifu.

Katika somo la pili, Petro analifananisha Kanisa na jengo la kiroho ambalo mjenzi ni Mungu na mawe yanayoishi ni watu. Msingi ulianza kwa mawe imara kwa jengo lote, Kristo ambaye juu yake Mungu ameweka pia mawe mengine, wale wanao mwamini yeye. Wakiwa wameunganika na Yesu, wanatengeneza hekalu moja la Mungu.

Injili inamuonesha Yesu kama kielelezo cha maisha ‘njia, ukweli na uzima’. Kiini cha ukristo ni Kristo mweyewe. Kazi yetu kwa Yesu na upendo wetu kwa watu, haijalishi tumeitwa katika maisha ya namna ghani, maisha yetu yanatiririka kutoka katika chanzo hiki. Mama Teresa aliulizwa kwanini alifanya aliokuwa akifanya, na alijibu tu “ni kwa ajili ya Yesu”. Hiki ndicho kiini kinacho shikilia ili kusiwe na mtikizo au usumbufu wowote. Ni muunganiko wa ndani na Yesu. Kusoma maisha yake, kupata muda wa kutambua mazingira yake na matukio ya maisha yake, kuwa familia na Injili na kumfahamu katika moyo wa sala, njia yetu ya kuweka msingi wetu na ujasiri wetu kuwa imara kwa Yesu. Hivyo mchague yeye katika hali zote za maisha kama Bwana wako na mkombozi. Kwa unyenyekevu jitambue kuwa bila yeye wewe si kitu, na jikabidhi kwake ili yeye aweze kukuongoza salama kwa Baba yetu wa mbinguni.

Sala: Bwana na Mkombozi, ninakukubali wewe katika maisha yangu kama Bwana na Mkombozi. Ninakushukuru kwa zawadi ya ubatizo iliyo anzisha maisha ya neema ninaomba nibadilishe maisha yangu niendelee kukufuata kikamilifu, leo na siku zote, ili uweze kuingia zaidi ndani ya maisha yangu. Ninaomba matendo yangu yote yaongozwe nawe ili niweze kuwa sadaka ilyio unganika na wewe milele, Yesu mpendwa. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni