Jumatano. 04 Desemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Julai 31, 2016

Dominika ya 18 ya Mwaka C

Mh 1: 2, 2:21-23;
Zab 90: 3-6, 12-14, 17;
Kol 3: 1-5, 9-11;
Lk 12: 13-21


MIMI, NAFSI YANGU, MIMI MWENYEWE!

Yesu anafuatwa na mmoja aliyekuwa katika makutano na anamtaka Yesu awe muamuzi kati yake na ndugu yake kuhusu ugawaji wa urithi wao. Yesu, lakini, alikataa kuingilia na kuwa muamuzi wa mambo yao lakini pia anatumia hali ile ili kuwafundisha wafuasi wake, juu ya tamaa ya kujilimbikizia na utajiri. Anawaambia, “angalieni na jihadharini na choyo”, kwakuwa uzima/ maisha ya mtu hayalindwi kwa wingi wa vitu alivyo navyo, na hata angekuwa na vingi kiasi ghani aisivyohitaji. Na hapo anaendelea kuelezea kuhusu mfano wa tajiri mmoja. Itambulike kwamba, huyu tajiri hajaoneshwa kama muovu, wala hajapata mali yake kwa njia zisizo halali au kwa kuwanyonya wengine. Haielezwi katika hali hiyo. Hakika, anaonekana kushangazwa na wingi wa mavuno yake na anafanya jambo ambalo linafikirika ili kuvuna mavuno ya shamba lake. Je, kosa lipo wapi? Tunaweza kujiuliza, kuna kosa ghani, kuhusu kujenga ghala kubwa ili kuhifadhi mavuno yake kwaajili ya baadaye?

Hamna, tunaweza kujibu, isipokuwa vitu viwili. Chakwanza, maswali aliokuwa anajiuliza yeye mwenyewe “Nifanyeje? Maana sina mahali pakuweka akiba mavuno yangu?” na pia alisema, “nitafanya hivi: nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi na hapo nitahifadhi mavuno na vitu vyangu vyote. Na nitaiambia nafsi yangu…..”. Anaisumbukia nafsi yake tu. Hana mawazo yakutaka kushughulika na kusaidia wengine, hakuna alama ya shukrani kwa Baraka alizo pata, hakuna utambuzi wa Mungu kabisa. Bwana shamba huyu tajiri ameangukia katika kuabudu kimungu ambacho ni maarufu sana: “utatu usio mtakatifu wa nafsi, wa, Mimi, mimi binafsi na mimi mwenyewe. Na la pili, anatabiri kuhusu wakati ujao, kwa hili ni mjinga si kwasababu anaongelea kuhusu wakati ujao bali ni kwasababu anadhani anawaze kutegemeza wakati ujao kwa mali yake.

Pamoja na ukuwaji wa teknologia wa millennia, pamoja na ukuwaji wa maarifa na akili au ukuwaji wa utamaduni, kila mwanadamu na ubinadamu bado unabaki kuwa dhaifu,tegemezi nakuweza kuharibika. Maisha ya mwanadamu katika hali hii yanasumbuliwa na, kutokuwa na uhakika, kukosa ulinzi napengine kwasababu hii tunakazana kujitafutia ulinzi na kujikinga dhidi dharoba za maisha kwa kupitia nguvu na kazi zetu.

Je, tunapigana vipi na vishawishi vya kutaka kushikilia, kulinda na kujilimbikizia mali ya ulimwengu huu? Kwanza, ukiwa umepewa zaidi, kuwa mtu wa kutoa kwa wengine pia. Kwakutoa kunaleta furaha ambayo utajiri hauwezi kununua. Paulo anatuambia tutenge fedha kila wakati tuweze kutoa kama Bwana anavyotujalia (1 Kor 16: 1-2). Tambua kwamba ni vitu vichache vya milele na jiwekee hazina katika hilo. Jiulize mwenyewe “Nini ninachotaka kuchukua niende nacho wakati nitakapo kufa?”. Vitu ambavyo tunaweza kwenda navyo Mbinguni ni ushuhuda wa watu ambao tuligusa maisha yao kwa njia ya Injili. Hazina ya Kimungu. Kama tutapanga maisha yetu katika vitu vya umilele, hapo tutakuwa tunafanya sahihi kuhusu maisha ya wakati ujao. Na tatu, kama una vingi au vichache, vishikilie katika hali ya wepesi. Usiweke matumaini yako yote katika vitu, vinaweza vikaondoka vyote kutoka katika mikono yako. Mshikilie Mungu daima. Hataondoka ndani mwako milele.

Sala: Bwana, ponya ugonjwa wa “Mimi mwenyewe” ndani mwangu. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni