Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Imani Kubwa!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Jumamosi ya 18 ya Mwaka → Kum. 6: 4-13 · Zab. 18 :1-2, 46, 50 · Mt. 17: 14-20
Katika Injili ya leo, baada ya wanafunzi wa Yesu kurudi katika utume wao, walishangaa kwanini hawakuweza kumponya kijana aliyekuwa ana pepo mchafu. “kasababu ya Imani yenu ndogo” Yesu aliwaambia. Mngekua na Imani ndogo kama chembe ya haradani” aliwaambia, “hakuna chochote ambacho kingeshindikana kwenu”.Mwaliko huu wa Yesu sio kiingiilio cha kumpa rushwa Mungu atafanyie maajabu, bali ni mwito wa kuweka matumaini yetu yote kwake kwa chochote kitokeacho kwetu, yeye tayari ajua lipi bora kwetu kulingana na mapenzi yake.Imani hii ikiwa ndani ya upendo mkuu, ndio iletayo furaha na amani katika maisha yetu, hata katika kipindi kigumu cha maisha yake.

Sala:
Ee Bwana, Nakutumainia wewe.
Amina.
0 Maoni

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni