Jumatano, Machi 22, 2017
Jumatano, Machi 22, 2017.
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
Kumb 4:1, 5-9
Zab 147: 12-13,15-16,19-20;
Mt 5:17-19
YESU: UTIMILIFU WA SHERIA
Masomo ya leo yanatupa picha kuhusu sheria ya Mungu. Ni za taratibu na kamilifu. Yesu alifanya kurejea “sheria na Manabii” akisema kwamba hakuja kutengua sheria za manabii bali kuzitimiza. Zilikuja kutimizwa baada ya miaka elfu na zaidi. Ilichukuwa muda kwa utimilifu wa mpango wa Mungu kujifunua. Lakini ulijifungua kwa wakati wake na kwa jinsi yake. Ni hakika, wale wote waliokuwa katika Kipindi cha Agano la Kale walikuwa na shauku ya Masiha kuja ili kutimiza vitu vyote. Nabii baada ya nabii alikuja akinyoosha kidole mbele kwa wakati ujao kwamba Masiha atakuja. Hata sheria za Agano la Kale katika hali Fulani zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaandaa watu wa Mungu kwa ajili ya ujio wa Masiha. Lakini ilikuwa ni hali ya taratibu ya kutengeneza sheria, kuziweka kwa watu wa Israeli, kuwasaidia ili kuzielewa, na kuanza kuziishi. Hata Masiha alivyokuja, kuna wengine kwasababu ya shauku na furaha walitaka atimize yote kwa wakati mmoja. Walitaka Ufalme wao wa dunia uanzishwe na walitaka Masiha wao mpya achukue Ufalme wake.
Lakini mpango wa Mungu ni tofauti kabisa na hekima ya Binadamu. Njia zake zilikuwa tofauti kabisa na njia zetu. Na njia zake zikaendelea kuwa mbali kabisa na njia zetu! Yesu alitimiza kila sheria katika Agano la Kale na Manabii, na si kama vile watu walivyokuwa wanadhani. Wayahudi wakati wa Yesu walikuwa wamejikita mno katika sheria binafsi na mapokeo katika sheria ya Musa kiasi kwamba walipoteza picha halisi. Iliwawia vigumu kumtambua Yesu kwamba yeye mwenyewe ndiye mtimilifu wa sheria, kwamba alikuwa sheria ya Mungu iliochukuwa umwilisho. Kwa maneno yake na matendo yake alileta sheria katika maisha. Sio tena mlolongo wa Maandishi, sheria sasa zilikuwa kitu cha kuishi katika uhalisia na kila mtu alihisi. Tafakari kwa kujitafiti mwenyewe kama nawe ni mtu wa kuangalia tu karibu kama Wayahudi! Je, unamuona Yesu kama anayeishi na mtilifu wa sheria?
Sala: Bwana, ninakabidhi maisha yangu kwako. Nina amini kwamba una mpango kamili kwangu na kwa watoto wako wapendwa. Nipe subira niweze kukusubiri wewe na nikuache wewe ulete mapenzi yako ya Kimungu yatimie katika maisha yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina
Maoni
Ingia utoe maoni