Jumatatu, Machi 13, 2017
Jumatatu, Machi 13, 2017.
Juma la 2 la Kwaresima
Dan 9:4-10
Zab 79:8-11,13
Lk 6:36-38
USIHUKUMU!
Ulishawahi kukutana na mtu kwa mara ya kwanza na bila hata kuongea na huyu mtu mara moja unahitimisha unayofikiri juu yake au wao? Kama sisi wenyewe ni waaminifu ni lazima tukiri kwamba ni rahisi kuhukumu watu wengine kwa haraka. Kilicho kigumu ni kubadilisha hukumu yetu tuliojiwekea kuhusu hao wengine. Ni vigumu kuwahukumu tukiwapa mafanikio na kuondoa wasi wasi wetu na kufikiri ni wazuri.
Yesu alivyosema “usihukumu nawe hauta hukumiwa” anatualika sisi tusiwe watu wa kuwahukumu watu katika hali yeyote. Ulimwengu unahitaji watu wengi wasio hukumu na wala kulaani. Tunahitaji watu wanao fahamu kutengeneza urafiki na kuleta upendo usio na masharti. Na Mungu anataka wewe uwe mmoja wao wa hao watu. Tutafakari ni mara ngapi tumekuwa watu wakuwahukumu watu, na tutafakari ni kwa namna ghani sisi ni wazuri katika kutengeneza urafiki na wale wote walio karibu yetu. Mwishowe, kama tumekuwa watu wa kutengeneza huu urafiki, ni wazi tutapokea Baraka kutoka kwa wengine wanao tupatia na sisi urafiki kama huo. Na kwa njia hiyo sisi wote tutabarikiwa.
Sala: Bwana, ninaomba unipe moyo usio hukumu. Ninaomba unisaidie niwapende wote ninao kutana nao kwa mapendo matakatifu na kuwakubali. Ninaomba unipe mapendo ya kweli na urafiki wa kweli kwa wengine ili niweze kuamini na kufurahia upendo unaopenda mimi niwe nao. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni