Jumanne. 03 Desemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Oktoba 18, 2024

Ijumaa, Oktoba 18, 2024,
Juma la 28 la Mwaka wa Kanisa

Sikukuu ya Mt. Luka Mwinjili,

2 Tim 4:10-17
Zab 144:10-13, 17-18
Lk 10: 1-9


TUMEITWA KUWA MASHAHIDI WA YESU!

Katika Injili, Luka leo anatuonesha tena wengine sabini ambao Yesu anawatuma baada ya kupokea maelekezo. Luka lazima atakuwa pia ni mmoja wapo wa Wafuasi waliotumwa kwa utume. Ni vigumu kwa mtu ambaye hakuwa karibu na Yesu kufahamu namna hiyo na kuweka katika mpangilio katika kumwelezea kama mtu mkamilifu.

Sisi pia maagizo haya yanatolewa kwetu. Tunapaswa kujitoa kwa ufahamu wetu wote kuhubiri Ufalme wa Mungu na sio kuyumbishwa na vitu vingine vidogo. Kufanya haya ni lazima kusafiri na mwanga-chukua tu, vile vya muhimu na tuacha nyuma yote ambayo yanaweza kutuharibu. Tunakaribishwa kufanya kazi hii, si kwasababu ya chochote tutakachopata kutokana nayo, bali kwa yale tutakayo wapa wengine bila malipo, bila kutegemea heshima Fulani au malipo flani. Bwana anataka wafuasi wake wamtegemee yeye na sio kujitegemea wenyewe.

Sala:
Bwana, naomba furaha na ukweli wa Injili ubadili maisha yangu ili niweze kuutoa ushuhuda kwa wale wote walioo karibu name.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni