Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Watakatifu: Wito wa Watu Wote wa Kuwa Watakatifu!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Sherehe ya Watakatifu Wote → Ufu 7:2-4,9-14 · Zab 24:1-6 · 1Yoh 3:1-3 · Mt 5:1-12
Watakatifu ni wale walio jitahidi kuishi hapa duniani kadiri ya thamani ya Injili. Hata baada ya kifo chao wanaendelea kuwa mfano na mashuhuda wa Injili kwa wale waliobaki dunaini. Wakiwa wameumbwa wakiwa na mwili na damu kama sisi walitamani kupata utakatifu. Hawa ni wale waliopata moyo kutoka kwa watakatifu wengine wakisema “kama yeye amekuwa mtakatifu kwanini mimi nisiwe?” Watakatifu mbinguni wana bahati ya kuwa mbele za Mungu daima. Walio wengi wakiwa bado hapa duniani walifurahia kuwa ndani ya Mungu daima wakiwa hapa duaniani. Mginguni ni pale alipo Mungu, na Mungu yupo ndani ya mioyo yetu, kwahiyo walikuwa na Mungu daima mbinguni. Watakatifu waliishi wakilijua hili na wakajikuta wakiwa katika furaha ya Mungu daima.

Injili ya Leo inatualika kufuata zile heri kama njia ya kuelekea kupata Utakatifu. Sisi ni nani tuishi maisha ya utakatifu? Mt. Augustino alijikuta akipata ugumu wakuishi heri hizi, lakini alisoma maisha ya watakatifu na akasema, “ Kama hawa watu wakawaida waume kwa wake waliweza, kwanini mimi nisiweze?”

Sala:
Bwana, umetuita kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni. Tuwekee ndani yetu hamu ya kukufurahisha wewe kwa kila kitu na utufundishe njia ya ukamilifu.
Amina
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni