Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Agosti 19, 2024

Jumatatu, Agosti 19, 2024
Juma la 20 la Mwaka


Ez 24: 15-24
Lumb 32:18-21;
Mt 19: 16-22


TUNAITWA KUWA MASKINI WA ROHO

Tunaishi katika ulimwengu ambao ni rahisi kuchukuliwa na mali au vitu na hivyo kupoteza muelekeo wetu na wa wengine. Sisi twaweza kuingia katika kujali mali kuwa ndio mwisho wa kila kitu. “kama unataka kuwa mkamilifu, uza vyote ulivyo navyo na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Alafu, njoo unifuate”. Wakati kijana huyu mdogo alivyo sikia hivyo alihuzunika sana kwani alikua na mali nyingi.

Yesu anawaita baadhi ya watu katika hali ya kawaida wauze vyote walivyo navyo. Na wote wale wanao tambua wito huu na kujitoa katika kuacha kushikamana na mali, wanapata uhuru mkubwa. Wito wao ni alama ya ndani ya kila mmoja wetu, wito wa ndani ambao kila mmoja wetu amepewa. Lakini kwa wengine je, Bwana anawaitaje? Ni kwa kuwa maskini wa roho. Kwa kuwa “maskni wa roho” ni katika hali hiyo Bwana alikuwa anawaalika kuachilia yote ya malimwengu na kuacha kujifungamanisha nayo, kama hawa waliofanya katika hali ya vitendo. Tofati iliopo ni kwasababu wito wa mmoja ni wa ndani na wa njee, na wengine ni kwa ndani tu. Lakini inapaswa kuwa kamili.

Umaskini wa roho ni kwamba tunatambua Baraka tunazozipata kwa kujinasua kwa kutokushikamana na mali za ulimwengu huu. Mali sio mbaya. Lakini ni rahisi kushikwa na vitu vya ulimwengu. Mara nyingi tunakuwa na vishawishi na kufikiri kwamba kadiri tunavyokuwa na mali nyingi ndivyo tunavyokuwa na raha zaidi. Lakini sio kweli, “aliye na vingi hatosheki”.

Tafakari leo juu ya wito ulioitiwa wa kuishi huku Ulimwenguni bila kujifunganisha na mali. Mali na vitu vingine ni ishara tu ya njee ya kukusaidia kupata uzima wa milele katika malengo ya maisha. Na hili litakuwa na maana kwamba utapata unayo hitaji na kukwepa kuwa na vingi, na hasa kukwepa kujishika na malimwengu kutoka ndani.

Sala:
Bwana, ninatamani kuacha yote yanayo nifunga. Ninajitoa kwako kama sadaka ya kiroho. Pokea yote niliyonayo na nisaidie mimi niweze ku tumia katika hali ambayo wewe mwenyewe unatamani. Katika kuachilia huko niweze kuvumbua utajiri wa kweli ulioniwekea mimi. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni