Jumatano. 30 Oktoba. 2024

Tafakari

Jumatano, Agosti 21, 2024

Jumatano, Agosti 21, 2024,
Juma la 20 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mtakatifu Papa Pius X

Eze 34:1-11;
Zab 22:1-6;
Mt 20:1-16


KUWA MUWAJIBIKAJI!


Neno la Mungu linaongea nasi kuhusu kuwajibika, na kwanamna ya pekee, majukumu yaliowekwa juu yetu na Mungu. Katika somo la kwanza, Mungu anawakumbusha viongozi wa wana Waisraeli kuwa wao ni wawajibikaji wa matatizo na mateso ya watu. Walichaguliwa kuongoza watu, kuendana na amri zake. Lakini, wanawaongoza katika kuvunja uhusiano wao na Mungu kwakuharibu taratibu za kidini, nakuwachanganya kati yao ili waweze kujinufaisha binafsi kifedha na kisiasa. Na hili lime sababisha uharibifu na kupelekwa uhamishoni. Ezekiel anawaeleza kuhusu kushindwa kwao kuwa wachugaji wema wa watu.

Sisi wote pia, katika hali Fulani, tumewekwa kuwa wachungaji au wahudumu juu ya wengine. Kama Padre, Mtawa, Wazazi, Walimu, viongozi wa serikali, tunapaswa kutimiza majukumu yetu yakuwahudumia watu waliowekwa chini yetu au wanao tutegemea. Somo la kwanza linatueleza kwamba watu hawa hawapo chini yetu ili kuwahujumu au kuwaonea bali ni watu wa Mungu waliowekwa chini yetu na Mungu ili tuwahudumie. Hii inamaana kwamba sisi tupo na tutabaki kuwa wawajibikaji wa Mungu.

Somo la Injili ni juu ya mfano wa wafanyakazi wa shamba la mizabibu walio ajiriwa nakufanya kazi kwa masaa tofauti bali wanapewa mshahara sawa. Kitu kimoja cha kweli ambacho mfano huu unatufunulia ni kwamba, kwakuangalia majukumu yetu aliotupa Mungu, Mungu haangalii umefanya kazi muda mrefu kiasi ghani, bali anaangalia ni kwa jinsi ghani tumetenda kazi kwa uaminifu na kwa majitoleo. Hatimaye, hata kama tuna kazi ndefu na majukumu marefu katika maisha kama ya wazazi au kama ya mwalimu anayefundisha wanafunzi kwa kipindi kifupi, tunapaswa kuwa sawa katika kuitenda hiyo kazi kiaminifu na kwa majitoleo. Na majitoleo yetu ya kujitoa kwetu kutakuwa kwa hali ya juu na hapo tutaambiwa-“njooni kwangu mliobarikiwa na Baba yangu, muurithi ufalme mliotayarishiwa kabla ya kuumbwa misingi ya ulimwengu” (Mt 25:34).

Sala:
Bwana, nakuomba unisaidie niweze kuwa mchungaji mwema wa kundi lililowekwa chini yangu, niweze kutimiza majukumu yaliowekwa chini yangu.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni