Jumapili, Juni 30, 2024
Jumapili, Juni, 30, 2024
Tafakari ya kila siku
Juma la 13 la Mwaka wa Kanisa
Hek 1:13-15; 2:23-24
Zab 30:1,3-5,10-12 (K. 1);
2 Kor 8:7,9,13-15;
Mk 5:21-43.
JE, UMEPOKEA GUSO LA YESU?
Tuanze tafakari yetu kwa mfano ufuatao, Kijana mmoja alianza safari yake ya kutokea Morogoro kwa miguu kuja Mbagala Zakheim (Dar es salaam) akatembea, akatembea, Muda mrefu mnoo, akafika Chalinze, akaendelea na safari yake akawa anakaribia Mlandizi lakini alipokuwa akikatiza katika pori fulani aliona haiwezekana Mbagala ikawa sehemu ya mwelekeo wa pori au Dar es salaam iwe katika maeneo haya au mwelekeo huu. Akaamua kurudi mpaka Chalinze na kuamua kuchukua ile barabara ya kuelekea Moshi. Unaweza kufikiria anataka kwenda Mbagala Dar es salaam. Sijui ataipata lini? Ndugu zangu sisi pengine Imani yetu imekuwa hivi. Tunasali Sanaa tena tunajitahidi kwenda kanisani kila siku na huenda tunamuomba Mungu atuponye katika ugonjwa fulani , au hitaji fulani, lakini ile tunakaribia kupona/kulipata au pengine Mungu anataka kuleta uponyaji sisi nasi tunakata tamaa, tunaamua kurudi nyuma na hali yetu inakuwa mbaya zaidi. Wakati mwingine tunapokea ushauri mmbaya na kuona bora nigeukie kwa Waganga na kumuacha Mungu wakati umesali muda mrefu sana na Mungu ndiyo anataka kuleta Baraka na wewe unaamua kubalidilisha njia na kurudi dhambini, subira na uvumilivu katika sala ni muhimu. Yairo angesikiliza ushari wa ndugu wa nyumbani mwake pengine angekosa uponyaji kutoka kwa Yesu wa binti yake.
Katika Injili ya leo, tanakutana na miujiza miwili ambapo Yesu. Kwanza anamponya yule mwanamke mwenye kutoka damu, halafu baadaye anamfufua binti ya Yairo. Miujiza hii mwili inatufundisha kwamba Mungu, katika Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, hawezi kuruhusu woga, au magojwa, au mauti itoe neno la mwisho katika maisha yetu. Kwa imani yake katika Yesu yule mwanamke mgonjwa aligeuza woga wake ukawa ushujaa, na ugonjwa wake ukaponywa.
Yesu pia anamfufua binti wa Yairo na kumrejeshea uhai. Binti wa Yairo wa miaka kumi na mbili alikuwa anaumwa, na alilala katika kufa; akiwa ametishiwa na kifo chake , Yairo alitoka nje na kumfikia Yesu. Wakati Yairo alipomfikia Yesu, alianguka miguuni mwake Yesu na alimuomba aende nyumbani kwake, aliamini kuwa kama tu Yesu angekwenda nyumbani na kumuwekea mikono yake binti yake anayekufa, binti angepona. Baadhi ya watu kutoka nyumbani kwake walikuja na kumtaarifu Yairo kuwa binti yake mtoto alikuwa amekufa na hakukuwa na hitaji la kumsumbua Yesu juu ya hilo. Ndugu kutoka nyumba ya Yairo walimuangalia Yesu kuwa kama tabibu wa kawaida ambaye angeweza kufanya miujiza tu kama kungekuwa na uhai. Lakini hawakuwa na ufahamu kuwa ufalme wa Kristo na nguvu zake zilipita zaidi ya mipaka ya uhai na kifo. Yesu alimuuliza Yairo aendelee na imani yake – kuamini kuwa Yeye angeendelea kurejesha uhai wa binti yake, sio tu katika uhai, bali pia katika afya njema. Wakati Yesu alipokwenda katika nyumba ya Yairo, Aliushika mkono wa binti mdogo na alisema, “Msichana, nakuambia, Inuka,” na yule msichana alisimama. Muujiza ulikamilika; Yesu hakumfufua tu msichana toka mauti, bali pia aliiboresha afya yake. Kazi za Yesu daima ni kamilifu. Wakati anapotibu, anatibu kwa ujumla; na Anaposamehe, Anasamehe moja kwa moja. Imani kwa Yesu ni dawa yakutuponya sisi.
Kifo hakikubaliki katika tamaduni mbali mbali. Ingawaje kifo kinakuja kwetu katika njia mbali mbali. Kifo ambacho tunapaswa kuogopa ni kifo cha kiroho. Mungu alituumba sisi ili tuishi lakini kifo kikaja ulimwenguni. Kifo cha mwili. Kila mtu anaonekana kupigana na kifo cha kimwili. Kwetu sisi tunaomfuata Yesu, kifo cha kimwili ni lango lakuingia maisha ya milele, kwenda kuishi na Yesu milele.
Somo la kwanza leo nikutoka katika kitabu cha Hekima. Hata katika kitabu hiki tunasikia “Mungu alimuumba mtu si ili kumwangamiza”. Mungu alipenda sisi tuishi, lakini pia kifo kimekuja ulimwenguni. Somo kutoka Kitabu cha Agano la kale tayari wanatambua kwamba kifo sio jibu la mwisho kwa kuishi kwa Mwanadamu. Kifo ni jibu la mwisho kwa wale wanaoishi katika muungano na shetani.
Somo la pili kutoka katika barua ya pili kwa Wakorintho. Paulo anawashauri watu Wakorintho kuwa wakarimu kushirikisha hela kwa wale wasiokuwa na kitu. Hii ni hali nyingine ya kufa kwa nafsi ya umimi na kutambua kwamba tunapaswa kushirikishana kile tulichonacho ingawaje hatuna kingi. Tamaduni za sasa kweli watu wamekuwa wabinafsi mnoo na hata kushirikisha inakuwa ngumu sana. Na hii ni aina nyingine ya kuogopa kufa. Tuna hofu yakuogopa kutokuwa na nayote tunayohitaji. Ni muhimu kutambua kwamba kila mara tunahitaji na tunachohitaji vinatofautiana, tunapaswa kuacha ubinafsi tutambue utofauti huu.
Hatunapaswa kutazama wengine wanaishije, bali mimi naishije. Tunapaswa kujitazama sisi wenyewe na kutambua kwamba sisi wenyewe tunakitu chakutoa na kutoa tulichonacho ili kuwasaidia wale wasio nacho. Mtakatifu Agustino alisema “tunapaswa kupigania nafsi zetu ziwe na kidogo ili wengine wawe na kingi zaidi.” Maneno hayo kwa ulimwengu huu bila Imani unaweza kumkimbiza mtu, ila ndivyo wana Wamungu wanavyopaswa kuishi. Tumuombe Mungu Imani hiyo.
Sala:
Bwana, Nisaidie niwe na ufahamu wa guso la Yesu katika Ekaristi Takatifu kila siku.
Amina!
Maoni
Ingia utoe maoni