Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Julai 03, 2024

Tafakari ya kila siku
Jumatano, Julai 3, 2024
Juma la 13 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Tomasi Mtume.

Ef 2: 19-22;
Zab 116: 1-2;
Yn 20: 24-29.

KUTOA USHUHUDA KWA YESU MFUFUKA!

Leo tuna sheherekea sikukuu ya Mt. Thomasi, Mtume. Thomas ni maarufu sana kwa maswali yake aliyeyaleta, na tunaweza kutulia kwasababu ya maneno ya kwanza aliyosema Yesu, wakati Tomasi akiwa na mashaka: “Amani iwe nanyi”. Yesu hakumwaibisha au kupatwa na hasira bali alimpa Amani. Yesu ambaye anatufahamu sisi katika ubinadamu wetu na ambaye anatufahamu undani wetu kabisa, anatupatia sisi amani wakati tukiwa katika hofu na mashaka yetu. Wakati Thomasi anatoa ishara kwa ajili ya ombi lake la kuingia katika hali hiyo ya Imani au kuamini, haombi kitu kigeni zaidi ya ile Imani ambayo kila mfuasi alikuwa ameshapokea. Ni wazi kwamba yeye alitaka kupata naye muda wakushuhudia kama wengine walivyo fanya-kabla haja amini jambo hilo kubwa linalo shangaza.

Lakini tukio haliishi hapa, kwa Yohane au kwa Bwana mfufuka mwenyewe anaendelea na kusema “je, una amini kwasababu umeniona? Wana heri wale wasio ona na kuamini”. Kwetu sisi maneno haya ni ya muhimu sana. Kwasababu hatukuona, sasa inakuwaje tuna amini? Tomasi hakuweza kuamini mpaka alipo ona. Petro hakuweza kaumini mpaka alivyo ona. Maria Magdalena hakuweza kuamini mpaka alivyo ona. Sasa tuta aminije wakati sisi hatujaona? Inawezekana kwasababu sisi tumesha barikiwa, “wamebarikiwa wale wasio ona lakini wana amini.”. Ni lazima tutambue na kukubali kwamba Imani yetu sio kutokana na juhudi zetu wenyewe au labda dini tunayo fuata bali ni “zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu”. Mungu Baba ametupa kitu ambacho kina saidia Imani yetu kwa Bwana mfufuka iwezekane-hata pale ambapo hatuja muona Yesu mfufuka kwa macho yetu ya kibinadamu.

Sala:
Bwana, imarisha Imani yangu kama Tomasi alivyolia “Bwana wangu na Mungu wangu”. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni