Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Julai 07, 2024

Julai7, 2024
Dominika ya 14 ya Mwaka

Eze 2:2-5
Zab 123 (K. 2);
2 Kor 12:7-10;
Mk 6:1-6.


KUTESEKA KWA NABII


Watu wengi ambao ni wakuu katika sehemu nyingi wamepeita mateso na changamoto mbali mbali na hivyo hata kuvishinda na kusimama imara. Huenda, watu wao wenyewe waliwakataa na walikuwa na wakati mgumu sana kuikabili jamii. Wale wote waliotumwa na Mungu nao pia wanakutana na magumu. Hata Mwana wa Mungu, ambaye watu walimsubiri kwa muda bado alipokuja walimpinga na hata watu wa nyumbani kwake hawakumuelewa.

Katika somo la kwanza, Ezekieli anakuwa kama chombo cha Mungu cha amani, akiwa kama balozi wa Mungu kati ya watu wake katika miaka hiyo kabla na baada ya Wayahudi hawajaanguka kwa Wababiloni. Manabii walipewa nguvu ya Roho wa Mungu kubainisha ukweli na haki na uaminifu katika hali ambayo sifa hizi zilifunikwa kwa uongo, ukosefu wa haki, na kutokuwa na imani kwa vizazi kadhaa. Unabii Wake ulikuwa katika hali husika ya kitaifa hususani ya kisiasa na ya kidini. Watu walikuwa wasumbufu kwasababu hawakutaka kumsikiliza Mungu. (Ez 3:7). “Usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao.” (Ez 2:6). Wanaweza wasiyaogope maneno yako, lakini walau “watajua yakuwa nabii amekuwapo miongoni mwao.” (Ez 2:5). Huu ni wito wa nabii. Ni mtu ambaye Mungu ameudhihirisha ukweli wake ili kuuwasilisha kwa watu wake.

Katika somo la pili, Paulo anaelezea upinzani wake. Inawezekana pia Paulo aliyafikiria matatizo mengi ya kichungaji yaliyolikabili kanisa la Korintho kama ni mwiba katika nyama yake. Mwanzo aliuliza kuwa mwiba huu utolewe kwake, lakini mwishowe aliukubali, na hata kutukuzwa katika kejeli, mateso, na magumu ambayo aliteseka nayo kwa ajili ya Kristo (2 Kor 12:10).

Katika Injili, tunaona kukataliwa kwa Yesu na ndugu zake wa mitaa yake. Zaidi ya hili, Yesu alikutana na vikwazo kutoka katika mamlaka ya Wayahudi. Marko anahesabu muendelezo wa matukio matano ya upinzani ambapo Yesu ilimpasa ajitetee yeye mwenyewe: nguvu yake ya kusamehe dhambi (2:1-12); upendo wake kwa watoza ushuru na wadhambi (2:13-17); mitazamo yake juu ya kufunga (2:18-22); uelewa wake juu ya usafi wa utamaduni (2:23-28); na nguvu zake za kuponya siku ya Sabato (3:1-6).

Katika Injili ya leo, ni kusanyiko la watu wa nyumbani ndio waliomsaliti Yesu. Alipitia kile walichokipitia Isaya, Yeremia na Ezekieli – yakuwa nabii hakubaliki nyumbani kwake. Ingawa watu wa Nazareti walifurahishwa sana na mafundisho ya kukubali asili yake ya miujiza na matendo yake, hawakuenda mbali na kushangawa kwao. Badala yake, waliishia kuoanza kutazama hali yake ya zamani na familia aliotoka. Badala ya kuwa na Imani wanaanza kuangalia mambo ya nje ambayo sio muhimu kwa wokovu wao. Wanashindwa kupokea ujumbe wa kiroho. Pengine nasi tunaweza kuwa kama watu wa Nazareti, tukawa tumejijengea kwamba unabii wa kweli hauwezi kutoka sehemu fulani au tukashindwa kupokea ukweli kwasababu tunadhani huyu hawezi kutuambia kitu. Pengine Padre fulani, ulimuona akikuwa au akiwa mseminari na sasa anakuhubiria unaanza kusema haka katoto kajuzi mbona nakifahamu vizuri hakina lolote? Tuangalie sana tusije tukamfukuza Yesu katika maisha yetu akashindwa kutenda miujiza akaenda kutenda miujiza sehemu nyingine.

Katika hali ya leo pia, hali haijabadilika. Tumeitwa kuwa manabii kwa watu wetu wenyewe, huenda ikahitaji kusimama kwa ajili ya matendo maovu ndani ya jamii, kuongea kwa ajili ya watu wasio na sauti au kuwatetea masikini na wananyanyaswaji. Tunapaswa kujiandaa na hata kutukanwa. Huu ndio wito wetu. Wito wetu wakushiriki katika unabii ya Kristo.

Sala:
Bwana, niimarishe mimi katika utume wangu kama nabii nihubiri ujumbe wako.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni