Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Julai 19, 2024

Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Julai 19, 2024
Juma la 15 la Mwaka


Isa. 38:1 – 6, 21 – 22, 7 – 8
Isa. 38:10 – 12, 16 (K) 17
Mt 12:1-8


KUSHIKA SIKU TAKATIFU YA SABATO!


Mitume wa Yesu walikuwa na njaa wakaanza kuvunja masuke ya ngano na kula ili kupooza njaa yao. Mafarisayo walianza kuwalaumu mitume wa Yesu kwani wanafanya kitu ambacho wao walikiita “kinyume na sheria” ya Sabato. Walisema kwamba kitendo cha mitume kukata masuke ya ngano na kula kilionekana ni “kazi” kiasi ambacho kinavunja sheria ya sabato ambayo watu hawapaswi kufanya kazi. Mitume hawakufanya kitu chochote kibaya ila walilaumiwa. Walikuwa watu wasio na kosa kama Yesu anavyosema. Yesu anawajibu Mafarisayo na hali yao yakutokufikiri vizuri kwa kuwakumbusha maandiko “nataka rehema na sio sadaka”. Anasema kwamba mitume wameonewa kwasababu mafarisayo hawakuelewa maandiko haya juu ya Huruma ya Mungu.

Sheria ya Sabato ya kupumzika ilikuwa imetoka kwa Mungu. Lakini sheria ya kupumzika haikuwa kwa ajili yake yenyewe. Siku ya sabato ya kupumzika ilikuwa zawadi kwa wanadamu kwani Mungu alijua Mwanadamua anahitaji siku ya kupumzika. Alitambua tunahitaji muda wa kupumzika katika wiki, kumwabudu Mungu na kuwa na wengine. Lakini mafarisayo waliigeuza siku ya sabato kuwa mzigo mkubwa. Waliifanya kuwa mzigo na hivyo kushindwa kuifanya iwe siku ya kumwabudu Mungu na kukutana na wengine.

Sisi huwa tunafanya hali yetu ya kujiona tumeelimika na kuwafanya watu waone kazi yangu au biashara yangu ndio maisha yote. Hali hiyo inakataliwa na kupingwa na siku ya Sabato. Kila siku ya sabato inatuambia kwamba sisi sio, vifaa bali ni watu. Hatupo ulimwenguni huku kutengeneza vitu na pesa, tupo ulimwenguni kujielimisha katika uzuri na urafiki na kumjua Mungu. Sabato inatukumbusha kwamba sisi sio mashine bali ni viumbee pekee vya kumtumikia Mungu. Sisi sio watu wabinafsi, bali watu tunaoshirikiana na kupendana. Hivyo katika siku hii tumkumbuke Muumba wetu na viumbe vyote katika siku hii. Tujiunge na viumbe vyote tumwimbie Mungu na kuifanya siku hii TAKATIFU!

SALA:
Bwana, nisaidie kupenda sheria yako. Nisaidie mimi niweze kuiona katika huruma na neema. Ninaomba niburudishwe kwa amri zako na kunyanyuliwa katika mapenzi yako. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni