Jumanne. 03 Desemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Julai 20, 2024

Jumamosi, 20 Julai, 2024
Tafakari ya Kila siku
Juma la 15 la Mwaka

Kut 12:37-41
Zab 136:1-10
Mt: 12:14-21


UTUMISHI WA YESU!


Neno kuu katika injili ya leo ni ‘tazama mtumishi wangu niliyemchagua.’ Kama Yesu alivyosema, hakuna ushahidi mkubwa kuliko ule wa Mungu baba kumshuhudia mwana; na huu ndio ushuhuda, kama ilivyoandikwa kwanza na nabii isaya, na kutafsiriwa na mwinjili mathayo. Lakini mtumishi mwaminifu wa Mungu anahukumiwa na watumishi wa uongo. Tunaona kuna mwendelezo katika hali ya taifa la israeli kumkataa Kristo. kuna mashaka, kupinga, kutojali na hatimaye kumkataa. Haya yote yanaongozwa na mafarisayo na waandishi wanaochukuliwa kuwa viongozi wa dini katika yerusalemu na Israeli. Tofauti na suluhisho lao baada ya baraza waliyokaa na kuamua kupanga namna ya kumwangamiza, roho wa Mungu alionesha maajabu na uzuri wa Kristo. Ndio kusema kuwa Mungu anamzungumzia Kristo toauti kabisa na ulimwengu unavyomzungumzia. Yesu angeweza kufanya chochote kujilinda dhidi ya washitaki wake, lakini huo haukuwa mpango wa Mungu. Alijitoa kabisa kufanya mapenzi ya baba yake. Akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Hicho ndicho kiini cha utumishiwake.

Sala:
Ee Bwana, nisaidie kukabiliana na upinzani na maadui zangu kwa upendo badala ya chuki na vita.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni