Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Julai 28, 2024

Julai 28, 2024,
Dominika ya Juma la 17 la Mwaka

2 Fal 4: 42-44;
Zab 145: 10-11, 15-18 (K) 16;
Efe 4:1-6;
Yn 6:1-15.


WOTE WAKASHIBA


Masomo ya leo hii yatusaidia kuadhimisha Yesu Kristo ambaye hutupatia chakula chetu cha kimwili na kiroho. Kwenye somo la kwanza, nabii Elisha anatabiri kwamba Mungu atawalisha watu wake kulingana na agano lake. “Uwape watu, ili wale; kwa kuwa Bwana asema hivi, Watakula na kusaza.” Yaani Bwana atazidisha chakula watu wake wale, washibe na waache mabakio.

Wimbo wa katikati, yamsifu Mungu ambaye kama Baba muumba ajali viumbe vyake vyote. “Macho ya watu wote yakuelekea wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, washibisha kila kilicho hai matakwa yake.”

Tukio ya nabii Elisha, anayefanya muujiza ili kuwalisha watu mia kwa mikate ishirini, ilitabiri Kristo ambaye, anafanya muujiza mkubwa zaidi, kwa kuwalisha watu wanaozidi elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili. Njaa zao za kimwili pamoja na za kiroho zote zilitosheka.

Yesu, anayaona mahitaji yetu na husikia kilio chetu. Anashirikisha uponyaji na matumaini na kumlisha kila mmoja kwa mkate na samaki. Hakuna mtu aliyeondoka bila ya kushibishwa. Kuna kingi zaidi kilichoachwa kwa ajili ya wale wote wenye uhitaji, “wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.” Katika maisha yetu, daima Mungu yupo katika vitu vidogo vidogo. Mungu anapatikana ambapo hatuwezi kujitegemea sisi wenyewe, na tunahitaji kumuamini. Mungu yupo zaidi tunapohangaika na kujikuta sisi wenyewe katika hali ya faraghani. Upendo wa Mungu ulipatikana juu msalabani, sehemu iliyojitenga zaidi kwa wote. Je, nasikia njaa? Je, naona kiu? Je, nataka kutosheka? Yesu mwenyewe aweza kutusaidia yote haya tukiweka matumaini yetu kwake.

Sala:
Bwana, Wafumbua mkono yako na wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni