Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Agosti 02, 2024

Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Agosti 2, 2024
Juma la 17 la Mwaka wa Kanisa

Yer 26: 1-9;
Zab 68: 5, 8-10, 14;
Mt. 13: 54-58.


UDONGO WENYE RUTUBA ILI KUPOKEA BARAKA ZA MUNGU


Yesu anaenda katika mji wa nyumbani kwake na kuhubiri habari njema lakini anakutana na upinzani wakutokukaribishwa kutoka kwa watu wake. Sio kwamba walikataa tu mafundisho yake na miujiza yake bali walitoa hukumu ambayo ni ya ajabu tena wakiangalia familia yake. “Je, huyu sio Mwana wa seremala? Mama yake sio Mariam”. Walimtazama kama mtu wa kawaida. Na hivyo wakazuia utukufu wa Mungu unaokuja kati yao.

Ujumbe huu wa Injili unatufundisha kwamba tunapaswa kuwa tayari kujifunza kwa wengine, hasa wale wanaofahamu hata kama tunawafahamu familia yao au tunamfahamu. Kwani Mungu anaweza kutufundisha sisi kupitia kwa ndugu wa familia zetu. Kingine tunapaswa kuchelewa au kutokuhukumu mtu kwa kutazama historia ya familia yake au mambo yake ya zamani. Hakuna mtu ambaye anabaki kama alivyo daima. Tunapaswa kuwatazama watu kwa mtazamo mpya na mtazamo mpya. Tatu, kila wakati tunaposikia neno la Mungu likitangazwa kwetu, tunapaswa kusikiliza sio kwa kutazama mtu bali kutazama Roho Mtakatifu aneyeongea kupitia yeye. Nne, usikatishwe tamaa na watu kutokupokea neno la Mungu wala usikubali kuangushwa na mtu ambaye hataki kukufuata. Zaidi sana usiache kuwatendea mema wengine.
Matendo matukufu ya Mungu hayakuweza kutendeka kule Nazareti kwasababu ya kukosa kwao Imani. Watu walikuwa na mioyo migumu wakashindwa kuruhusu mioyo na akili zao zipokee neno la Yesu. Kwa njia hii Yesu hakuweza kufanya miujiza mikuu maeneno ya nyumbani kwake.

Je, unamruhusu Yesu akufanye uwe mpya siku kwa siku? Je, unamruhusu yeye atende mambo makuu katika maisha yako? Kama utakuwa na mashaka katika swali hili ni ishara kwamba Mungu anataka kufanya makuu katika maisha yako.

Sala:
Bwana, ninakuomba moyo wangu uwe na rutuba kwa ajili ya kazi yako kuu. Ninaomba moyo wangu ufanywe upya nawe, maneno yako na uwepo wako katika maisha yangu. Njia katika maisha yangu na unifanye upya chombo cha neema yako. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni