Jumatatu, Februari 27, 2017
Jumatatu, Februari 27, 2017.
Juma la 8 la Mwaka wa Kanisa
YbS 17: 20-24;
Zab 32: 1-2, 5-7;
Mk 10: 17-27
KUJIBU WITO WA YESU!
Katika Injili ya leo, Yesu anamuangalia “kijana tajiri” na “anampenda”. Yesu anamwitia kuachia kila kitu alicho nacho, kutoa yote na kumfuata yeye. Yesu alimwalika afanye hivi kwasababu ya upendo. Yesu anamwita huyu kijana ili aweze kupata mengi zaidi kuliko yale aliokuwa nayo. Ndio maana Yesu alimtazama kwa mapendo kabla hajamwita huyu kumfuata katika hali ya kuacha yote kabisa. Lakini katika hali hii ya huyu Yesu anayependa inaumiza. Ilikuwa inaumiza katika hali kwamba kumfuata huyu Yesu ilihitaji sadaka ya kila kitu. Ilikuwa ni kujikana na kuachia yote. Ilikuwa ni ngumu katika hali ya kibinadamu na hali ya kidunia. Lakini upendo wa Yesu kwa huyu kijana ulikuwa kamili kiasi kwamba ulikuwa umsaidie huyu kijana kuachia yote na kupata mengi zaidi. Lakini kama ilivyo kawaida kwa Mungu, anapenda kumpa mwanadamu uhuru achague mwenyewe ka uhuru wake kamili.
Tunaitwa kufanya hivyo pia. Tunaweza tusiitwe kumfuata Yesu katika hali ya kuacha yote katika hali ya mali tulionayo. Lakini tunaitwa katika hali ya kumfuata Yesu katika hali ya kumwamini hakika na kujikabidhi kwenye mapenzi yake. Na kwa njia ya mapenzi yake haiwezekani bila sadaka. Sadaka katika hali ya juu.
Majibu yetu ya jinsi ya kufuata wito wa Yesu ni muhimu. Ni namna ghani tunaitikia wito huu wa Yesu na kujitoa kabisa kwake? Huyu kijana tajiri alijibu kwanza kwa huzuni. Hakukubali wito aliomwitia Yesu. Mara nyingi hali hii imekuwa majibu yetu. Tunataka kumfuata Yesu katika hali ya uaminifu bila kujali anatuamuru nini. Lakini tunapopewa hali halisi ya kujibu wito wake, tunarudi nyuma kwa huzuni kwakufikiria wito huo unagharimu mno.
Tuangalie, angalia maisha yako binafsi na angalia ni kwa jinsi ghani ulivyo tayari kusema “ndio” kuachia vyote kwa jinsi Yesu atakavyo kuambia. Kwa kusema “ndio” katika hali ya sadaka ni uamuzi mzuri kabisa ambao unaweza kufanya. Katika hali ya kweli, ni uamuzi wa kweli uliokubalika wa hali ya utukufu ambao mtu anaweza kuishi.
Sala: Bwana, kukufuata wewe inawezekana ikaonekana kuwa ngumu na kugharimu. Inawezekana kuwa kama inazidi mno. Nisaidie hasa katika hali hizi, nikuamini wewe zaidi ya yale yote nilio nayo katika ulimwengu huu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni