Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Mei 26, 2024

Jumapili, Mei 26, 2024
Sherehe ya Utatu Mtakatifu

Kumb 4: 32-34,39-40;
Zab 33: 4-6,9,18-20,22 (K.13);
Rum 8:14-17;
Mt 28: 16-20.


MUNGU KATIKA UTATU


Wakatoliki, duniani kote, sio kwamba wanaamini Mungu tu, bali wanaamini Mungu mmoja. Lakini Mungu wetu yupo katika Utatu- Utatu katika umoja na umoja katika Utatu. Kila mmoja ni Mungu kwa asili na wote ni Mungu mmoja. Sawa katika Nguvu, ni wa milele na wana utukufu. Fumbo hili kuu linaweza kuchukuliwa kama fumbo lililo kuu kabisa katika Biblia Takatifu. Wakristo tunaamini fumbo hili kuu ndani ya mamlaka ya Yesu Kristo na Agano Jipya. Ni moja wapo ya fumbo kubwa la ndani kabisa lililofunuliwa na lililopo juu kabisa kupita akili ya mwanadamu. Yesu mara nyingi ameongea kuhusu Mungu kama Baba yake. Sauti ya Baba ilisikika wakati wa ubatizo wa Yesu; “Huyu ni mwanangu mpendwa niliye pendezwa naye msikilizeni yeye”. Yesu alipo ngara sura, pia, sauti hiyo hiyo ilisikika ikisema maneno hayo hayo. Katika matukio yote uwepo wa wingu jeupe ilionyesha uwepo wa Roho Mtakatifu, ambaye Yesu aliwaahidia wakati alipokuwa akipaa kwenda kwa Baba, “nitawapa msaidizi Mwingine-Roho wa kweli anayetoka kwa Baba”.

Yesu anatuambia kwamba, Mungu aliupenda sana ulimwengu mpaka akamtuma mwanaye ulimwenguni, ili wote watakao muamini wasipotee bali wawe na uzima wa milele (Yn 3:16). Anaelezea uhusiano wake ndani ya Mungu mmoja wa kweli na anawataka mitume na wafuasi watambue na wakubali kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwamba Mungu ni Baba yake, na kwamba Roho Mtakatifu alitumwa kwao na Baba na Mwana. Wakristo wa kwanza walisadiki ndani ya Utatu Mtakatifu bila kupinga. Baada ya kuamini, kinachofuata ni Upendo. “Kama mtu akinipenda mimi” Yesu anasema, “Baba yangu atampenda. Nasi tutakuja kwake nakufanya makao ndani yake.”

“…(Wana ndoa) matunda ya wana ndoa yanakuwa ishara ya kuelewa na kuelezea fumbo la Mungu mwenyewe, kwasababu kwa mtazamo wa Kikristo wa Utatu mtakatifu, Mungu anatafakariwa kama Baba, na Mwana na Roho Upendo. Utatu Mtakatifu ni umoja wa upendo, na familia ndiyo inayoishi kuonesha umoja huu. Mtakatifu Papa Yohane Paulo wa Pili, alitoa mwanga kwa hili alivyosema ‘Mungu wetu katika undani wake sio upweke bali ni familia, kwani ndani yake ana Ubaba, mwana na undani wa familia ambaye ni Upendo. upendo huo ndani ya familia ya Kimungu ni Roho Mtakatifu’”. (Baba Mtakatifu Fransisko katika Furaha ya upendo, Amoris Laetitia, 11)

Tutafakari leo juu ya sherehe hii ya Utatu Mtakatifu, ni mara ngapi nina enzi upendo huu wa Utatu Mtakatifu katika mahusiano yangu? Tujaribu kufanya jitihada tusonge mbele zaidi, katika mapendo yetu, na kumruhusu Mungu akupe matokeo mazuri ya tokanayo na upendo wako kwake na kwa jirani.

Sala:
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, nisaidie mimi niweze kuku fahamu wewe na kukupenda. Nisaidie niweze kuelewa upendo unaoshiriki na Mwanao. Kwa kuelewa upendo huo, nisaidie na mimi niweze kushirikisha upendo huo kwa wengine. Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni