Ijumaa. 18 Oktoba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 01, 2024

Jumamosi, Juni 1, 2024,
Juma la 8 la Mwaka wa Kanisa

Yud 17:20-25;
Zab: 62: 2-6;
Mk 11: 27-33


KUMUONA MUNGU KATIKA MAISHA YETU!

Yesu sasa yupo Yerusalemu. Katika Injili ya leo, wakati Yesu akiwa anatembea hekaluni, walimuendea viongozi na wazee Wawayahudi, Makuhani, walimu wa sheria na Wazee. “nikwa mamlaka ya nani unatenda haya?” walimuuliza Yesu. Hii ikimaanisha kwamba hafanyi katika hali ambayo inaonesha kujali mamlaka yao. Kama ilivyo ada kwa Yesu, anawauliza swali na wao. Aliuliza kama kazi ya Yohane Mbatizaji ilitoka kwa wanadamu au kwa Mungu.

Wakatambua mara moja kujibu Swahili la Yesu ingewaletea matatizo. Kwa udhaifu mkubwa wanajibu, “hatujui”. Jibu lisilo lakawaida kabisa tena lisiloridhisha na ajabu kabisa tena kutoka kwa viongozi wakubwa wa kiroho wa watu. Hapo Yesu akakataa kuwajibu swali lao walilokuwa wameuliza awali. Hali ya Yesu inafanana na ile ya Yohane Mbatizaji. Watu waliomsikia Yesu akiongea (“hakuna aliyewahi kuzungumza namna hii”) na kuona anavyoponya watu (“Mungu amewajia watu wake”), hawakuwa na wasiwasi wowote juu ya mamlaka yake. “Watu walishangazwa na mafundisho yake, kwani alifundisha kwa mamlaka sio kama Walimu wa sheria” (Mk 1:22). Swali la viongozi wa Wayahudi ilidhirisha kabisa udhaifu wao na upofu wao kwenye jambo ambalo lipo wazi lisiloweza kufichika machoni pa watu wote.

Sisi pia tunaweza kuwa na upofu huo. Tunaweza tukakataa kuona uwepo wa kazi ya Mungu katika hali ambazo sisi wenyewe hatutaki kuona, katika watu ambao hatutaki kuwaona, au kuwadharau baadhi ya watu na kuwaona kama hawana chochote chakuweza kuniambia pengine kwasababu ya elimu yao au udhaifu wao. Lakini tutambue Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote, jambo lolote, zuri au lisiloonekana zuri machoni petu, ili kuleta ujumbe wake.

Sala:
Nisaidiye Bwana, kukutafuta na kukupata na nitende yale yote unayotaka nitende katika Maisha yangu.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni