Jumapili. 08 Septemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Juni 03, 2024

Jumatatu, Juni 3, 2024,
Tafakari ya kila siku
Juma la 9 la Mwaka wa Kanisa

2 Pet 1: 2-7;
Zab 90: 1-2, 14-16;
Mk 12: 1-12


MUNGU ANAYETUJALI (MWEMA)!


Fumbo tulilo nalo leo kwa tafakari yetu ni kuhusu muonekano wa uzuri na wema wa Mungu. Jinsi Mungu anavyotenda na jinsi mwanadamu anavyofikiri ni vitu viwili tofauti kabisa kiasi ambacho mwanadamu anajiandaa akidhani atashambuliwa. Wema haujajikita katika kutoa mengi tu, bali kutoa hata kidogo kwa wakati. Mungu alimtoa Mwanaye kwawakati kwa ajili yetu. Alitupa yote kwa wakati. Yesu aliongea na kutenda katika hali ambayo watu kwakuona anayosema nakutenda, wakatambua Mungu ni wa namna ghani. Kwa maneno mwengine, Yesu hakuongea tuu kuhusu Mungu na kuonyesha muelekeo wa kwenda kwake, bali alionesha uwepo wa Mungu na Mungu akaonekana akiwa kati ya watu wake. Kama sio yeye, Mungu kwetu angekuwa ni kama kitu tuu cha kutumaini nakutafuta. Lakini kwa njia yake Mungu yupo kati yetu (Ekaristi Takatifu). Kabla ya Yesu, hakuna aliyejua sifa za Ufalme wa Mungu ulivyo, yeye ndiye aliyetupa mifano akielezea jinsi Ufalme wa Mungu ulivyo, na akatuambia yeye amekuja kuutangaza, upo kati yetu, na bado utatimilizwa katika maisha ya umilele. Kwahiyo tukiishi vizuri na wengine tunaishi Ufalme wake tukiwa hapa duniani.

Yesu, hakutaka chochote kwa ajili yake binafsi, bali kila kitu alichokuwa nacho na kutenda, alifanya kwa ajili ya wengine. Kila mmoja wetu ni wa Yesu, chombo cha upendo wa Mungu, na chombo chakupokea wema wa Mungu. Leo tujiulize kama tumekuwa wazi kwa wema na upendo huu wa Mungu.

Sala:
Nisaidie Bwana, niweze kuutambua wema wako ili niweze kuwa mwema.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni