Jumatano, Juni 05, 2024
Jumatano, Juni, 5, 2024,
Tafakari ya kila siku
Juma la 9 la Mwaka wa Kanisa
2 Tim 1: 1-3, 6-12;
Zab 122: 1-2;
Mk 12: 18-27.
MIMI NI UFUFUO NA UZIMA!
Somo la kwanza la leo linatuonesha jinsi ghani Mtume Paulo alivyo elewa kwamba Injili inaweza kuhubiriwa kwa mataifa yote tu, kwa nguvu ya Yesu mfufuka. Kwa kujikita kwenye faida yetu, au vipaji vyetu au nguvu zetu wenyewe maisha yatakuwa kama balbu ya umeme isiokuwa na umeme. Hitaji la sasa nikumtumikia Bwana wetu kwa moyo safi tukijikita katika ahadi zake za uzima wa milele alizo tuachia Yesu mwenyewe.
Katika somo la Injili Yesu anatuambia ni wale tuu wanao elewa maandiko matakatifu na nguvu ya Mungu wataamini katika ufufuo wa wafu. Hili lilikuwa jibu kwa swali lililoulizwa na Masadukayo. Yesu anawajibu kwamba mambo ya ndoa ni mambo ya dunia hii. Baada ya kufa tunakuwa kama malaika wa mbinguni. Yesu kwa njia ya ufufuko wake ameyashinda mauti na kutupatia uzima wa milele. Yeye ni Bwana wa uzima. Maisha yetu yapaswa yamwelekee yeye zaidi, tukitazamia lililo kubwa zaidi kuliko maisha yetu ya dunia, tukijua uzima wa milele ndio lengo letu baada ya maisha haya. Tusifungwe na malimwengu tushindwe kumuona Mungu baada ya maisha haya. Kwa mfano wa mfiadini Mt.Yustino tujifunze kutoa maisha yetu kwa Kristo mfufuka ili tuweze kupata lile taji lisilofifia (uzima wa milele).
Sala.
Bwana Yesu, hatuweze kuwa Wakristo wenye kuzaa matunda mema kama tutajitenga nawe. Tunaomba utusaidie tuweze kupata kitambulisho chetu, kuishi kwetu na maisha yetu kutoka kwako.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni