Jumapili. 08 Septemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Mei 24, 2024

Ijumaa, Mei, 24, 2024,
Juma la 7 la Mwaka wa Kanisa

Yak 5:9-12;
Zab 103: 1-4, 8-9, 11-12;
Mk 10:1-12


KIFUNGO CHA NDOA


Nafikiri, njia nzuri ya kuinjilisha nikuwaongoza wengine kwakuwa mfano. Wana ndoa wazuri Wakristo wanaweza kuwa wainjilishaji wazuri katika ulimwengu mzima, kwasababu mwanga wao utawaangazia wengine (Mt 5:16). Katika liturjuia ya leo inatupeleka katika uchaguzi muhimu ambao wana ndoa wanafanya katika maisha yao, ambao ni NDOA. Lakini pia, tunaona ndoa nyingi na familia nyingi zilizovunjika katika mazingira yetu. Katika Injili Yesu anasema, tangu mwanzo haikuwa hivyo (Mt 19:4).

Katika kitabu cha Mwanzo katika Biblia (chenye maana ya Mwanzoni) kina tuambia; ilikuwa ni mpango wa Mungu kwamba mwanamume awe na msaidizi (Mw 2:18). Mwanamke alikuwa kiumbe tofauti kabisa na viumbe vingine vyote alivyo viumba Mungu, kwamba, aliumba wanyama na ndege kutoka ardhini (Mw 2:19) lakini mwanamke aliumbwa kutoka ubavu wa Adamu (Mw 2:22). Kwahiyo katika ndoa mwanamume akiacha yote anaungana na mke wake nakuwa mwili mmoja.

Kama ilivyo katika miito mingine, wito wa ndoa ni uhuru wa mtu, ambapo mwanamke anamchagua mwanamume au mwanamume anamchagua mwanamke na kuweka naye maagano kwamba wataishi wote kwa maisha yao. Lakini magumu, na taabu ni sehemu ya maisha ya kila mtu na yapo katika wito wowote. Sasa tufanyeje? Mtakatifu Yakobo katika somo la kwanza leo, anatukumbusha tuwe na upole, kuchukuliana na kuwa imara na sio kulalamika kila wakati. Kwasababu Bwana aliyejiunga nanyi atawasaidia muweze kuishi pamoja (Mk 10:9). Uaminifu katika ndoa unadhihirisha uaminifu alio nao Mungu kwa watu wake. Yeye ni mwaminifu daima na atatusaidia kubaki waaminifu.

“Hakuna familia iliyokamilifu iliyodondoka chini kutoka mbinguni, familia inatakiwa kukuwa kila mara na kukomaa katika upendo. Huu ni wito usio isha uliozaliwa ndani ya umoja uliyo katika Utatu Mtakatifu, umoja uliyo kati ya Yesu na kanisa lake, jumuiya ya upendo ambayo ni familia ya Nazareti, na umoja uliopo kati ya watakatifu wa Mbinguni” Baba Mtakatifu Fransisko katika, “Furaha ya Upendo” (Amoris Laetitia).

Sala:
Bwana wajalie wana ndoa ujasiri wakuonesha mfano wa uaminifu. Tunaomba sisi sote tuwasaidie wana ndoa wanaojitahidi kutoka katika hali yao ya maumivu na mateso waweze kuishi tena kwa uaminifu na upendo.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni