Jumanne, Aprili 30, 2024
Jumanne, Aprili 30, 2024,
Juma la 5 la Pasaka
Mdo 14: 19-28;
Zab 145: 10-13, 21 (R. 12);
Yn 14: 27-31.
AMANI YA KRISTO INAYO FARIJI!
Wakati Yesu alivyo anza utume wake, wafuasi wake walimwamini kuwa mtu maalumu, na wakaacha kila kitu hata familia zao, miji yao ya nyumbani. Waliamini kwamba Yesu atapindua utawala wa Kirumi na kuanzisha utawala wa utukufu wa Daudi. Kuamini huku kulifungwa na Yesu kwa kuwaambia juu ya mateso na kifo.
Yesu alitambua kukazana kwao na mateso na wasi wasi wao, na nikatika mioyo hii iliyojaa wasi wasi Yesu anawaambia “msifadhaike mioyoni mwenu…..amani na waachia ninyi”. Ni amri ya mapendo kutoka kwa Bwana wetu. Anataka kuwahakikishia kwamba hofu na mioyo iliojaa wasi wasi sio ya watu wake. Kuwa na hofu na wasi wasi ni mzigo mkubwa sana unaoweza kutuangusha chini. Yesu anatu hakikishia kabisa kwamba tunapaswa kuwa huru kutoka katika hali kama hii. Anataka sisi tuwe huru ili tuweze kufurahia furaha ya maisha.
Hatua ya kwanza ya kuwa huru ni kutambua mzigo ni upi. Kuutambua na kutafuta sababu ya mzigo huo. Kama sababu ya mzigo wako ni kwasababu ya dhambi zako, zijute na fanya bidii kuziungama. Hii ni njia bora kabisa ya kuhisi uhuru wa ndani. Lakini pengine mzigo wako ni kwasababu ya matendo ya mwingine au hali Fulani ya maisha ambayo yapo chini ya uwezo wako, hapo upo katika hali ya pekee ya kuikabidhi kwa Bwana wetu, kumpa hali yote ya kumiliki hali yote. Uhuru unapatika katika hali ya kujikabidhi kabisa, kuamini na kujikabidhi katika mapenzi yake. Yesu anataka tuwe huru ili tuweze kuhisi furaha anayotaka kutupatia katika maisha yetu. Tunaomba Amani ya Kristo itiririke katika mioyo yetu na kwa njia yetu, na kukutana na wote tunao kutana nao.
Sala:
Bwana, ninataka kuwa huru. Ninataka kuhisi furaha ulionayo kwa ajili yangu. Wakati mizigo ya maisha inapo nielemea, nisaidie niweze kukugeukia daima ukiwa msaada wangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni