Jumatatu. 13 Mei. 2024

Tafakari

Ijumaa, Februari 24, 2017

Ijumaa Februari 24, 2017,
Juma la 7 la Mwaka wa Kanisa

YbS 6: 5-17;
Ps 119: 12, 16, 18, 27, 34-35;
Mk 10: 1-12.


NDOA, WITO MTAKATIFU!

Wana ndoa wazuri wa Kikristo wanaweza kuwa chanzo kizuri cha uishilishaji kwa ulimwengu mzima, kwa sababu mwanga wao utawaangazia wengine (Mt 5:16). Lirtujia ya leo inatuletea kutafakari kuhusu uchaguzi sahihi tunaofanya katika maisha, hasa ndoa. Kwa ujumla ndoa zetu zinafanyika katika hali ya haraka haraka, bila kuwa na muda wakutafakari. Matatizo mengi yanakuja baada ya ndoa, magumu mengi yanajitokeza baada ya ndoa, ambayo yanaishia kwenye talaka. Hii haina maana ya kubaki uchumba sugu kwa kigezo cha kutafakari wala sio kubaki katika dhambi kwa kisingizio cha kutafakari na kumchunguza mtu. Mwaweza kubaki katika hali ya neema kila mtu akiwa nyumbani kwake huku mkitafakari na kumwomba Mungu juu ya maamuzi mnayotaka kufanya. Lakini pia itambulike shida na changamoto zitabaki kuwepo daima katika ndoa tunachopaswa kufanya ni kufanya kila jitihada kuziondoa kwa kushirikiana kwa upendo, shida yeyote isiwakimbize kutafuta talaka au utengano wa namna yeyote bali iwafanye muungane zaidi ili muweze kuitatua na kuishi kwa amani.

Katika Injili ya leo Yesu anasema, “tangu hapo mwanzo haikuwa hivyo” (Mt 19:4), kwa hiyo ilikuwa je? Kitabu cha Mwanzo (chenye maana ya mwanzo) kinatuambia. Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu kwamba Mwanaume apate msaidizi (Mwa 2:18). Mwanamke alikuwa tofauti na kitu kingine chochote alicho umba. Aliwaumba wanyama wa porini na ndege kutoka ardhini (Mwa 2:19) lakini mwanamke alimuumba kutoka katika ubavu wa Adamu (Mwa 2:22). Kwa hiyo mwanamume atacha yote na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.

Kama ilivyo kwa miito mingine, ndoa ni juu ya uhuru wa mtu mwenyewe, ambapo mwanamke anamchagua mwanaume au mwanamume anamchagua mwanamke na kuahidiana kupendendana na kuwa pamoja kwa maisha yote. Lakini ugumu, na kipindi kigumu ni sehemu ya kila mmoja wao. Uaminifu katika ndoa unakuwa unaiga mfano wa uaminifu wa Mungu kwa watu wake. Yeye ni mwaminifu daima na atawasaidia kubaki waaminifu.

Sala: Bwana, saidia ndoa zilizopo waweze kuwa mfano kwa kizazi cha wadogo kinachokuja, kinacho fikiria talaka kama tamaduni. Tunaomba waonesha katika dunia kwamba uaminifu katika ndoa unawezekana na una matunda na kwamba sio makubaliano ya muda, bali ni ukweli wa daima. Yesu tunaomba wana ndoa wakutumainie wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni