Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Aprili 21, 2024

Tafakari ya Pasaka
Aprili 21, 2024.

------------------------------------------------
JUMAPILI, DOMONIKA YA 4 YA PASAKA MWAKA B

Somo la 1: Mdo 4:8-12 Petro akijazwa Roho Mtakatifu anasema, “uponyaji wa kiwete yule ulifanywa na Yesu mfufuka ambaye walimuua hapo kwanza.”

Wimbo wa katikati : Zab 118:1,8-9,21-23,26,28-29 Ni vyema kumtumainia Bwana kuliko kutegemea wanadamu.

Somo la 2: 1 Yn 3:1-2 Yohane anawaambia wakristo wa kipindi hicho na sisi kwamba sisi ni watoto wa Mungu tukiwa tunaishi kwa uzima wa Kimungu ambao upo ndani ya Mungu.

Injili: Yn 10:11-18 Yesu anawambia maadui wake na sisi kwamba yeye ni Mchungaji mwema anaye wafahamu kundi lake, anampenda kila mmoja na yupo tayari kufa kwa ajili yao.
------------------------------------------------

KUKUTANA NA MCHUNGAJI MWEMA!

Tazama ni upendo wa namna gani alionao Baba kwetu kwamba sisi tuitwe wanawake na kweli ndivyo tulivyo (Somo la 2). Kila mmoja anapaswa kutafakari juu ya maneno haya wakati maneno haya yakiwa yanazama ndani ya mioyo yetu. Yohane anaongea kuhusu wewe na mimi! Je, mimi ni mtoto wa Mungu? Ndio, hilo nimefunuliwa kweli. Uzima ulio katika maisha ya Kimungu katika Utatu Mtakatifu upo ndani yetu, ni uzima wetu pia. Uhusiano wetu huu ni sehemu ya adhimisho letu leo.


Jumapili ya nne ya Pasaka inajulikana kama jumapili ya Mchungaji Mwema, kama Yesu anavyo jiongelea mwenyewe kuwa ni “Mchungaji mwema”. Yesu anatupa sura ya Mchungaji mwema anaye wafahamu kondoo wake: anawaita, anawalisha na kuwaongoza. Ni kwasababu ya hili Kanisa limeipendekeza kuwa siku ya kuombea miito duniani.

Yesu anaonesha wazi tofauti ya wachungaji. Tofauti anayotoa ni juu ya mchungaji yule anaye wafahamu kondoo wake na kuwajali, na wale wanaofuata tu mkumbo bila sadaka ya upendo. Yesu alitolea sadaka kamilifu kama Mchungaji wa Kimungu. Alikuwa yupo tayari kutembea nasi katika njia zote, sisi kondoo wake. Alikuwa yupo tayari kutoa sadaka ya kila kitu. Hakutaka mateso, kuonewa, kukataliwa na mambo mengine yamuondoe kutoka katika lengo lake la kuwajali na kuwatunza watu wake katika njia kamili. Inapaswa ituguse na sisi, kutufariji na kutupatia sisi ujasiri na kutambua ni kwa jinsi ghani upendo wake ulivyokuwa mkubwa kwetu.

Wakati upendo aliotoa mmoja kwa ajili yetu ni kamili, tena wakati wa wakati mgumu, huu ni msaada mkubwa. Na upendo unaotolewa kwa mwingine kama huu unatengeneza muunganiko wa kiroho ambao ni imara kuliko matatizo tunayo weza kukutana nayo. Haijalishi ni kitu ghani kigumu kinachoweza kuja katika njia zetu, tunapaswa kutambua upendo na msaada usio na kikomo kutoka kwa Mchungaji wetu mwema. Na kama tunaweza kuona upendo huo kamili kutoka kwa wengine, tunakuwa kweli tumebarikiwa mara mbili. Katika hali nyingine Yesu anaongea kuhusu mfano wa mtu mwingine ambaye sio mchungaji mwema, ambaye anaona mbwa mwitu wakija na yeye hukimbia. Tunapaswa kuona ndani ya mtu huyu, vishawishi vyote ambavyo vyaweza kuja katika maisha yetu. Ni vigumu kubaki wakati wa nyakati ngumu. Ni vigumu kuwa karibu na wale wenye shinda wanapo tuhitaji sisi. Ni vigumu kuwa waminifu mpaka mwisho bila kuwa na aibu tunapo kutana na vishawishi vya hofu. Yesu anatupa nguvu na msaada wa upendo kamili yeye akiwa kama Mchungaji wetu mwema, lakini pia anatuhitaji nasi turudishe upendo huu huu kwake, kwa kuwapatia wengine upendo huu huu mkamilifu. Pale ulipo shindwa na kupungukiwa tunamuomba yeye akuchunge kama mchungaji ili nawe uweze kuwachunga wengine. Mkimbilie mchungaji mwema na amini upendo wake kwako.

Leo, Kanisa zima linatukumbusha hitaji letu la kuomba, kama Yesu mwenyewe alivyo waambia wanafunzi wake, hivyo kwamba "mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake" (Lk 10: 2). Tangu hapo awali Kanisa “ kwa asili yake ni umisionari" (Ad Gentes, 2), wito wa Ukristo unazaliwa ndani ya watu kutokana na kazi ya umisionari. Kusikia na kufuata sauti ya Kristo Mchungaji mwema, maana yake ni kuruhusi tuvutwe naye na tuongozwe naye, kujiweka wakfu kwake maana yake kumruhusu Roho Mtakatifu kututumia sisi katika mabadiliko haya ya umisionari, na kuamsha ndani yetu tamaa, furaha na ujasiri wa kutoa maisha yetu wenyewe katika utumishi wa Ufalme wa Mungu.

Katika mzizi wa kila wito wa Kikristo tunaona harakati hii ya msingi, ya kuacha nyuma faraja yetu na mambo yote yanayo tupendezesha nafsi zetu na kujikita katika maisha ya Yesu Kristo. Ina maana ya kuondoka, kama Abrahamu, na kuacha sehemu yetu ya asili na kwenda mbele kwa uaminifu, tukijua kwamba Mungu atatuonesha njia ya nchi mpya. Hii "kwenda mbele" isi tazamwe kama ishara ya mpango tu wa maisha ya mtu binafsi, hisia ya mtu, utu wa mtu mwenyewe. Kinyume chake, wale ambao wanamfuata Kristo wanapata uzima kwa wingi kwa kujiweka wenyewe bila kujibakiza katika utumishi wa Mungu na ufalme wake. Wito wa Kikristo kwanza kabisa ni wito wa upendo, upendo ambao hutuvuta sisi na kutuelekeza nje ya sisi wenyewe. Kuitika wito wa Mungu, maana yake kumruhusu yeye atusaidie kujiacha wenyewe kwakuondokana na usalama wetu wa uongo, na kutoka nje na kuenenda kwenye njia inayo ongoza kwa Yesu Kristo, aliye asili na hatima ya maisha yetu na furaha yetu.

Katika siku hizi kwanza tunaombwa tuombee Kanisa liweze kupata wachungaji wema na waadilifu wa kufanya kazi ya Kristo ya kueneza Injili, na kwamba Kanisa liweze kupata vijana wengi wanoitwa kwenye wito wa upadre na utawa ikiwa ni pamoja na watoto wetu wenyewe.

SALA:
Baba wa huruma, uliyemtoa mwanao kwa ajili ya wokovu wetu na ambaye anatutia nguvu kila wakati kwa zawadi ya Roho wako, tujaliye sisi jumuiya ya Wakristo tulio hai, upendo na furaha, vilivyo vya muhimu kwa maisha ya kindugu, na vinavyojenga ndani ya wadogo mwamko wa wito wakujitoa wenyewe wakfu kwako na kwa ajili ya wito wa uenezaji wa neno lako. Dumisha ndani ya jumuiya hizi majitoleo ya kutoa katekesi ya kuitika wito huu wakujitoa wakfu kwako. Wajaliye hekima inayohitajika katika maamuzi ya kufuata wito wako, ili katika yote ukuu wa huruma yako ya upendo iweze kungara. Tunaomba Maria, Mama na uliyekuwa kiongozi wa Yesu, utombee. Yesu tunakutumainia wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni