Jumapili, Aprili 14, 2024
Aprili 14, 2024.
------------------------------------------------
JUMAPILI, JUMA LA 3 LA PASAKA
Somo la 1: Mdo 3: 13-15, 17-19 Petro anaongea na watu wa Yerusalemu, akiwaambia kwamba wametenda kwasababu ya ujinga wao kumuua Yesu, na anawaalika wajirudi.
Wimbo wa Katikati: Zab 4: 2, 4, 7-9 Siku hii imefanywa na Bwana, tufuraha na kushangilia.
Somo la 2: 1 Yn 2; 1-5 Yohane anaeleza kwamba lengo lake la kuandika nikuwasaidia watu watoke katika dhambi, lakini kama wakianguka, Yesu atawasamehe wakimrudia.
Injili: Lk 24: 35-48 Yesu anawatokea mitume, akiwapa uhakika kwamba kweli amefufuka anawaalika wamguse, akiwapa uhakika kutoka katika maandiko kwamba Masiha lazima alikuwa ateseke na kutangaza toba kwa mataifa yote.
------------------------------------------------
KUKUTANA NA YESU MFUFUKA KATIKA MAISHA YETU
Yesu mfufuka amejaa aina za kushangaza. Uwepo wake unaleta Amani na furaha. Anashirikisha maisha yake mapya na rafiki zake. Kumbukumbu yake na maneno yake yameendelea kuwashangaza wengi hata siku hizi. Kufufuka kwa Yesu kunafanya sasa mitume waanze maisha mapya, kunawafanya watafiti maisha yao na kuanza maisha mapya ya upendo. Wanachukua mwanga wa pasaka na kuupeleka katika giza la ijumaa kuu na sasa mambo yanakuwa tofauti. Ni Yesu mfufuka tu anayeleta maana ya mambo yaliopita. Kwa maneno yake na kwakuumega mkate mambo ya zamani yanaletwa kwenye maana halisi. Mambo ya zamani yanaletwa kwenye mwanga na kutafsiriwa kwamba Yesu ni kweli mfufuka na kwamba ni Bwana.
Kulikuwa na dereva wa treni ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuendesha kwenda na kurudi kila siku katika njia hiyo hiyo. Kila siku kazi ilikuwa ni kitu cha kawaida kiasi ambacho aliweze kufanya hii kazi akiwa amefunga macho. Alikuwa na muda mwigi wa kuona mengi. Kulikuwa na hiki kinyumba ambacho kilimvutia sana. Kilikuwa kimejengwa mbali kidogo na njia ya treni. Kilikuwa kama kitu ambacho mtu anaweza kusema kwamba kinaweza kuwa tu kwenye kadi kama picha. Akakipenda sana “ooh sehemu nzuri ilioje kuishi?” alisema, “ooh pengine siku moja nikistaafu kazi nitaishi sehemu kama hii” alijisemea.
Siku moja mchana alipita pale akamuona mtoto mmoja wake akicheza mbele ya kile kinyumba. Yule mtoto akampungia wakati treni ilivyokuwa inapita. Akapiga honi kama kujibu. Siku iliyofuata ikatokea tena hivyo hivyo. Na hapo kukaanza urafiki kati yake na yule mtoto. Kila mchana alikuwa pale akimpungia na yeye anapiga honi kumrudishia. Wakati mwingine huyu mtoto alijikuta pia yupo na Mama yake pale na hivyo walijikuta wakimpungia mkono wote na dereva kurudisha kwa honi. Kitendo hiki kilimfanya dereva awe na furaha sana. Kilifanya pia safari ya kila siku inayochosha kuwa fupi. Kila wakati alikuwa anasubiria kuwaona na kuwapungia mkono. Kama ikitokea mmoja wao hajatokea alijisikia vibaya sana. Moyo wake ulipata huzuni na safari kuwa ndefu ya kuchosha. Miaka ikapita mtoto akakuwa. Pamoja na hayo siku nyingine ilikuwa labda Mama anapunga mkono au mtoto. Umoja ulitengenezwa kwa miaka bado ukaendelea. Na hivyo alistaafu akaenda kuishi sehemu ya mbali. Lakini hakuweza kusahau kile kinyumba na yule mtoto kutoka ndani ya akili yake. Hivyo siku moja akaamua kuwatembelea.
Alipofika karibu na nyumba ile mambo yalikuwa tofautri na alivyotegemea. Kuta za kile kinyumba hazikuwa nyeupe kama alivyokuwa akitegemea. nyufa zilikuwa zinaonekana. Yale maua hayakuwa mazuri kama alivyokuwa akifikiria. Kiukweli yalikuwa ya kawaida kabisa. Hata ile busatani ilikuwa na magugu makubwa tu kuzunguka ile nyumba. Miti ile haikuwa mizuri kama alivyodhani. Lakini mbaya zaidi alikata tamaa kabisa alivyokutana na yule mama na yule mtoto. Walikuwa wapole kwake alivyo waambia yeye alikuwa nani. Walimchukuwa katika sehemu ya kawaida kabisa na kuongea. Ilikuwa pia ngumu kuongea na kuhakikisha mazungumzo hayakatiki. Akajisikia vibaya. Hakuweza kueleza kwanini alikuja wala hawakutaka kujua kwanini amekuja. Kwahiyo kwa taratibu akaanza kuondoka pale. Alivyokuwa anaondoka akajisikia mtupu kabisa. Ndoto yake ikaishia katika ndoto hewani. Nyumba yake ambayo alikuwa amaeijenga ndani ya akili yake akaiona ikiishilia kutoka mikononi mwake kama mchanga unaokimbia kutoka katika mikono. Umoja uliokuwa umekuwepo kabla kati yao nae, ambao ulimpa maana saana katika maisha yake, ulifungwa hata hawezi kuurudisha. Lakini alivyokuwa akiondoka alitambua kwamba shida sio wao bali ni yeye mwenyewe.
Hatuwezi kusema kitu bali kumuonea huruma huyu dereva. Lakini je, haikuwa kosa kwake kuishi katika ulimwengu wa ndoto na kuacha kuishi katika maisha ya kweli? Ulimwengu wa ndoto kweli ulikuwa mzuri sana lakini ilikuwa ni hisia tu na kudhani. Lakini ni wazi kwamba hata ulimwengu halisi unaweza kuwa mzuri zaidi, kwasababu ni ukweli, kama angetoka na kwenda kutazama uhalisia.
Mara nyingi watu wengi wanashughulika na mambo ambayo hayapo katika uhalisi na kuyafuata kwa moyo wao wote. Wafuasi walifanya hivyo. Kwani kwa miaka mitatu walikuwa wakitegemea mambo ambayo hayapo katika uhalisia-Masiha ambaye hatakufa wala kuteseka, au kudharaulika na kufa. Na hivyo baada ya Yesu kufa, ulimwengu wa uhalisia ulionekana kwao na hivyo wakakata tamaa. Walianza kukata tamaa na kuwa na hofu. Hii sio njia nzuri ya kuishi. Mpaka tu pale mahali ambapo Yesu aliwatokea na kuwapa moyo na hivyo kuwarudisha katika uhalisi na ukweli wa Masiha. Ndoto zao zikabadilishwa na kuanza kugusa ukweli halisi. Ukweli ulikuwa ni kwamba kwa njia ya mateso yake na kifo cha aibu aliingia katika utukufu wake. Aliwaonesha vidonda vyake. Aliwaonesha waone wenyewe. Ilichukuwa muda kwa hili kuingia katika akili zaona pale ambapo akili zao zilielewa na kuingia kichwani walitambua kwamba sio wala kifo ambacho kinaweza kuvunja ule urafiki wao na Masiha wa kipindi cha miaka mitatu.
Ufukuo ni muhimu sana. Mbaya zaidi sisi tunakiona kama kitu ambacho kilitokea zamani na sehemu Fulani. Kama furaha za Paska niza kweli sisi pia tunaweza kukutana na Yesu mfufuka. Hatatutoa katika machozi yetu, na kutupeleka katika ulimwengu wa ndoto bali atakuwa nasi katika machungu yetu na kutuonesha kuelewa furaha na maana halisi katika huzuni hiyo.
Kwetu sisi ufufuko hautakuwa ni kitu kilichotokea kwa Yesu muda uliopita. Tunapokutana pamoja katika ekaristi tunakutana na Neno la Mungu na kuumega mkate pamoja. Yesu anakuja kwetu kwa nji ya neno na sakramenti kuja kutupa tumaini jipya na kutuongezea Imani juu yake. Tunapaswa kumwambia Bwana habari hizi na kumsikiliza yeye akiongea nasi, na kumtambua katika kuumega mkate. Nikwa njia hii tu tunaweza kutazama ya zamani kwa Imani na matumaini kwa mambo yajayo.
Sala:
Bwana, ninakushukuru wewe kwakutembea na mimi katika safari yangu. Ninakuomba nitambue maana ya ufufuko katika maisha yangu. Ninakuomba nikutane na wewe Yesu mfufuka katika maisha yangu.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni