Ijumaa. 03 Mei. 2024

Tafakari

Alhamisi, Aprili 11, 2024

Alhamisi, Aprili 11, 2024
Juma la 2 la Pasaka

Mdo 5:27-33
Zab 33: 2, 9, 17-20
Yn 3:31-36


KUJAA NEEMAA: NI KUISHI KATIKA KILE MUNGU ALICHOKUPA!


Wakati lipo tokea janga linalotokana na asili, au vita vya kisiasa, na chakula ni vigumu kupata, watu hushikilia na kupangilia kile walicho nacho. Na wasipofanya hivyo wanaona wanaweza kukosa chakula na kufa kwa njaa. Hivi kama Roho Mtakatifu ange tuambiae “nitawasaidia kwa kiwango fulani tu. Na kama ukimaliza neema zako, basi utajitambua mwenyewe” Mmm!

Kwa neema kwetu, Mungu hutenda tofauti kabisa na sisi. Anatupatia na kutumiminia Roho Mtakatifu katika hali yote na kutupatia neema zote tunazo hitaji. Shida ni kwamba hatuzitumii zote, na badala yake tuna acha kuzitumia. Hii si kwamba hatumwamini Mungu ni mkarimu. Bali ni kwasababu tunaogopa kumruhusu Mungu amimine nguvu zake katika maisha yetu.

Tujaribu kufikiria hivi maisha yangu yatafananaje nitakapo mruhusu Mungu afanye chochote anachopenda katika maisha yangu. Hivi, maisha yetu ya kila siku yangekuwaje, mahusiano yetu, maneno yetu na wakati wetu ujao hautakuwa tofauti? Tunatambua kuwa ni haki kumkumbatia Mungu katika kila kitu. Lakini inapofikia sasa ni wakati wa kukitenda, tunakuwa na wasi wasi mwingi. Inaweza kuwa ni wasi wasi wakitu kisicho julikana. Au kunaweza kuwa hatutaki kubadilika. Vyovyote inavyoweza kuwa Mungu anatupa neema zake zisizo pimika kwa kutumiminia Roho wake. Ni juu yako kuchagua kuamua kumsikiliza na kumchagua au unajipimia na kuchagua mambo mengine. Kumchagua Mungu ni jambo kubwa kuliko kitu chohcote unacho weza kufanya katika maisha yako.

Sala:
Bwana, ninataka wewe ufanye chochote unachopenda katika maisha yangu. Ninataka niingie kabisa ndani ya neema zako. Nisaidie niweze kusema “ndio” kwako bila kujali chochote kwa utukufu wa kusema “ndio” uliyo niitia. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni