Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Machi 21, 2024

Tafakari ya Kwaresima
Alhamisi, Machi 21, 2024
Juma la 5 la Kwaresima

Mwa17: 3-9;
Zab 104: 4-9;
Yn 8: 51-59.


AGANO LA UPENDO!

Lirtujia na Neno la Mungu linatualika sisi kukumbuka Agano la Mungu nasi kwa njia ya Yesu. Somo la kwanza linaonesha ukarimu wa Mungu akifanya Agano na Abram, na kuingia katika historia ya Mwanadamu. Ukuu wa Abramu umejikita katika Imani yake na utii kwa Mungu. Bila hata kujua Abram ana anza safari kwenda nchi asio ifahamu. Kwa kumuita Abram Mungu alibadilisha maisha yake yote. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Mwanadamu Mungu anabadilisha jina la mtu. Abram anaitwa Abrahamu. Ikiwa na maana kwamba Mungu anauwezo wa maisha yetu yote ya sasa na ya baadae. Agano la Mungu halifungwi tu kwa Abrahamu na familia yake tu. Kama mto unaotiririka daima limejaa ukarimu. Anacho taka Mungu kutoka kwetu ni kudumisha Agano hili daima.

Katika somo la Injili, Yesu anawaita watu waheshimu Agano la Mungu. Kama watalishika Agano hili hawataona mauti. Kwani kifo ni matokeo ya dhambi. Kwasababu ya kutotii Mwanadamu alipoteza heri machoni pa Mungu lakini Agano la Mungu kwa njia ya Yesu ni kuirudisha tena ile neema iliyopotea.

Sala:
Bwana, ninakuomba Moyo wako uweze kuchuja makosa yangu yote na kuruhusu mbegu ya ukweli kumea ndani ya akili na moyo wangu. Mungu wa Agano, tusaidie pia sisi tuweze kuwa waaminifu kwa maagano yetu nawe. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni