Jumatano, Machi 27, 2024
Tafakari ya Kwaresima
Jumatano, Machi 27, 2024
Juma Kuu
Isa 50: 4-9;
Zab 68: 8-10, 21-22, 31, 33-34;
Mt 26: 14-25.
KUBEBA MISALABA YETU!
“Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate." Mstari huu kutoka kitabu cha nabii Isaya unatukumbusha juu ya uchungu wa Yesu. Lakini, tunaweza kufikiria tu kile alichokihisi Yesu aliposoma maneno haya ya Isaya. Je, unafikiri maneno haya yalimpelekea awe na hofu? Au labda kwa sababu yeye alikuwa mwana wa Mungu, jambo hili halikumsumbua yeye kabisa? Pangine ukweli upo sehemu fulani kati ya hayo. Kuwa binadamu, Yesu kiasili alihisi matatizo makubwa juu ya kile kilichokuwa kikimngojea yeye. Lakini katika Umungu wake, aliweza kutamka kwa kujiamini sana, Bwana Mungu ndiye msaada wangu hivyo sina mashaka. Hivyo hakika alikuwa na hofu kubwa juu ya majaribu yaliopo mbele yake, vilevile Yeye alijawa na nguvu akijua kuwa Baba yake alikuwa pamoja naye na kamwe asinge mwacha.
Kuna uwiano hapa kwa maisha yetu. Hatuwezi kuona wakati ujao, lakini tunatambua kuwa tuna ugumu fulani waweza kuja katika maisha yetu na tunapaswa kuushughulikia. Pengine hatupo katika hali ambayo dhambi yetu inatuonesha tuna mkana Yesu moja kwa moja, lakini kila mmoja anaweza kuona aina fulani ya dhambi katika maisha yake. Tumia juma hili kwa uaminifu na kweli. Huruma ya Mungu ni ya ndani sana na njema mno, kiasi kwamba ungeielewa, kusingekuwa na haja ya kubaki na dhambi zako ukifikiria niungame namna ghani. Hali halisi haipo kama tunavyo ifikiria sisi wenyewe. Kama Yesu, tunajikabidhi kwa upendo na msaada wa Baba yetu wa Mbinguni. Tukiwa naye, ni hakika kwamba tunashinda tatizo lolote lile, kwani hawezi kuwatupa watoto wake.
Sala:
Bwana, ninaomba unisadie katika juma hili niweze kukabili dhambi zangu na udhaifu wangu. Mimi ni mdhambi, Bwana mpendwa, lakini inaweza kuwa vigumu sana kwangu kukubali ukweli huu. Ninaomba nikabidhi dhambi zangu kwako, ili niweze kuwa huru, na kupokea nafasi katika huruma yako kuu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni