Jumanne, Machi 19, 2024
Jumanne, Machi 19, 2024
Juma la 5 la Kwaresima
Sherehe ya Mt. Yosefu, Mume wa Bikira Maria.
2Sam 7:4-5,12-14,16;
Zab 89:2-5,27,29;
Rum 4:13,16-18,22;
Mt 1:16,18-21,24 au Lk 2:41-51
Mt. YOSEFU: MTU WA NDOTO NA MTU WA KAZI!
“Wakati Yosefu alivyo amka, alifanya kama malaika alivyo mwambia” (Mt 1:24). Haya maneno ya mwisho ya Injili ya leo, yanatupa muktasari mzima wa sherehe ya leo, ya Mt. Yosefu mume wa Bikira Maria. Maandiko yanatuambia kuwa Yosefu alikuwa mwana wa Yakobo na mume wa Maria na pia ni Mseremala kutoka Nazareth. Baada ya kumposa Maria, baada ya kutambua Bikira Maria ana mimba kabla hawajaanza kuishi pamoja, Yosefu akiwa ni mtu mwaminifu katika sheria, anaacha kumwaibisha Maria na ana azimu kumwacha kwa siri. Mungu aliongea naye kwenye ndoto na akatii. Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto na akafunua mpango wa Mungu kwa mwanadamu, na akamchukua Maria nyumbani kama mke wake.
Cha kuvutia, ni kwamba Yosefu hajaongea neno lolote katika maandiko (Injili). Bali ni mtu wa vitendo tu: anafanya alicho ambiwa na Malaika, anamchukua Maria kama mke wake na anaenda Bethlehemu: anatafuta sehemu ya kujihifadhi usiku, na anachukua familia yake Misri. Ingawaje sio matu wa maneno, lakini kwa hakika ni mtu wa matendo. Mungu alikuwa na mpango na Yosefu, na alikuwa tayari kuyafanya mapenzi ya Mungu. Alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akiyafuata mapenzi ya Mungu. Shauku ya maisha ya baadae, na vipingamizi vya nje havikumzuia kuacha kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Kwasababu alikuwa mwamini fu kutimiza mapenzi ya Mungu, Mungu alikuwa naye katika maisha yake yote.
Somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Samueli na pia wimbo wa katikati unatumbia kwamba Mfalme Daudi aliahidiwa kuwa mtoto wake ataishi milele. Daudi hakubaki mpaka kuiona ahadi hii ikitimia. Katika somo la pili, Paulo anawaeleza Warumi kuhusu Abraham, mtu mwingine mwenye haki ambaye hakuishi mpaka kuona matunda ya kazi yake. Alifanya mapenzi ya Mungu, lakini hakuona kutimia kwa ahadi ya Mungu kwake. Ingawaje hayakutimizwa kwa kipindi chake alitumaini na kuamini na Imani yake ilimpa kibali kwa Mungu. Katika somo la Injili tunamuona Yosefu mwenye Imani kwa Bwana. Alitembea katika majaribu mbali mbali kwa Imani. Aliamka kutoka katika ndoto na anakaanza kuweka kwenye matendo. Nini tunaweza kujifunza kutoka kwa Yosefu.
Utii kwa Mungu zaidi kuliko mwanadamu: sheria ilimwambia Yosefu kumwacha Maria na kumwacha aadhibiwe. Lakini hakusikiliza mawazo yake mwenyewe au kilichosemwa na sheria na watu. Yeye kwa nafsi yake anafuata mapenzi ya Mungu. Yosefu alikuwa mtu shujaa katika kumtii Mungu licha ya msukumo wa tamaduni. Je, jamii au Imani yangu inaleta mchango katika maamuzi yangu?
Wito ni muhimu kuliko kazi zetu: kwa Yosefu mpango wa Mungu maishani mwake ulikuwa muhimu zaidi kuliko mambo yake ya kijamii, kazi na familia. Yosefu yeye alikuwa Baba mume kabla yakuwa mseremala. Mungu wake, na familia yake ilikuwa muhimu zaidi kuliko kazi yake. Wito wake ulipita kazi zake. Je, familia yangu inakuwa muhimu zaidi kuliko kazi yangu? Familia inapaswa kuwa ya kwanza.
Mlinzi wa nyumba yake: Yosefu alikuwa mtu wa kuwa karibu na mke wake na kulinda familia yake. Anaitwa pia mlishi na mlinzi wa kanisa Katoliki. Watu walio mfano wa Yosefu ndio tunaokosa siku hizi. Watoto wetu wana achwa na kuingia kwenye hatari kama, mitandao, picha chafu, ulevi nk. Je, ni kwa jinsi ghani tulivyo walinzi wa familia zetu?
Mtu wa vitendo: Yosefu alikuwa mfanyakazi, na Mseremala. Hakuwa tu mtu wa ndoto, alikuwa mtu mchapa kazi, aliyepata chakula chake kwa uaminifu. Yosefu ni mfano kwetu kwa watu wanaopata chakula chao kwa kufanya kazi kihalali.
Yosefu ni mlinzi na mlishi wa Kanisa Katoliki, mlinzi na mlishi wa kanisa katika hatua za mwanzo, wakati kanisa lilipokuwa, Yesu, Maria na Yosefu. Tunafanya vizuri kumuiga Mt. Yosefu na kumuomba atuombee kama akina Baba wa familia walishi na walinzi. Mt. Yosefu utuombee..
Sala:
Bwana, tunakuomba tuwe watu wakuiga maisha ya Mt. Yosefu ili tuweze kuwa tayari kutimiza mapenzi yako bila kuwa na wasi wasi. Yesu nakumini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni