Jumanne. 07 Mei. 2024

Tafakari

Ijumaa, Machi 15, 2024

Ijumaa, Machi, 15, 2024,
Juma la 4 la Kwaresima

Hek 2: 1, 12-22;
Zab 34: 17-21, 23;
Yn 7: 1-2, 10, 25-30.


KUWEKWA MAJARIBUNI

Kitabu cha Hekima kina kadiriwa kuandikwa miaka mia kabla ya kuja Kristo. Lakini cha kushangaza maelezo yake yanaonekana kuwa karibu sana katika kumwelezea Yesu. Somo la leo linaongelea kuhusu mtu ambaye anamjua Mungu na hata anajiita “Mtumishi wa Mungu” (Hek 2:3). Na kama Yesu, huyu mtu ana adui ambao wanamfuatilia ili kumtega katika maneno yake na hata kutaka kumua. (2:19-20).

Leo tunakumbushwa kwamba kutakuwa na upinzani daima juu ya Kristo na wale wanao mfuata. Katika somo la Injili, tunasoma, juu ya kushindwa kwa jaribio la kumkamata Yesu wakati wa sikukuu ya Tabernaklo kwasababu “saa yake bado” (Yn 7:30). Ni kweli, Yesu alisulubiwa na kufa, lakini kifo hakikuweza kumweka chini. Mungu alimfufua! Ndivyo hivyo sisi Mungu hataruhusu kitu tunacho vumilia kituangushe bila kutusaidia. Atatuimarisha. Atatupa neema. Atatuinua tena.

Yesu anatuita sisi tuwe mabalozi wake. Anatutaka sisi tushirikishe habari njema kwa kila mtu tunae kutana naye. Huu ndio wito wa pekee, lakini pia kuna changamoto zake. Pengine juhudi zetu zitafanikiwa baada ya kupata upinzani mkubwa na majaribu makubwa, na hata changamoto nyingine ni za kusukumwa. Lakini tukibaki imara katika kushirikisha Injili kwa upendo na sio kwa kujiona wema wenyewe, kwa furaha na sio hasira, tutabarikiwa sana. Yesu atatuambia “vyema mtumwa mwema ingia katika furaha ya Bwana wako” (Mt 25:21). Hauhitaji kuwa mtu uliye bobea katika kuongea au kuwa mashuhuri katika kuongea. Wala haupaswi kuwa na nguvu labda nyingine. Tunapaswa kutambua tu Yesu anatupa nguvu na neema tunapo amua kumshuhudia. Na neema yake itatutunza kama ilivyo na nguvu ya kuwavuta watu kwake.

Sala:
Bwana, nakupenda. Nisaidie nikuone na kukupenda wewe katika jirani zangu. Nisaidie ninapo wekwa katika majaribu, na familia yangu, marafiki zangu, na wengine wanao nipinga kwasababu ya kukutangaza wewe na thamani ya Injili yako. Tufariji daima tunapo tangaza Injili yako. Tupe nguvu yako ya Kimungu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni