Jumatatu. 06 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Machi 16, 2024

Jumamosi, Machi 16 , 2024,
Juma la 4 la Kwaresima

Yer 11: 18-20;
Zab 7: 2-3, 9-12;
Yn 7: 40-53.


KUMSIKILIZA YESU

Ni vigumu kutokuitika unapokutana na ujumbe wa Yesu. Baadhi ya watu waliamini kuwa Yeye ni nabii, wengine kwamba ni Masiha, na hivyo walikuwa wameshawishika huenda ni mmoja wapo kati ya hao. Lakini muonekano wa wakuu unashangaza. Walienda kumkamata lakini wakarudi mikono mitupu, kwasababu hawakuwahi kumsikia yeyote akiongea kama yeye. Mafariyo na Waandishi wanaonekana kutopendezwa. Muonekano wa Nikodemu unaonekana kuwa ni wa woga. Moyo wake ulimwambia amlinde Yesu, lakini akili yake ilimwambia asije akajihatarishia maisha.

Wakati Yesu anafundisha kuna kitu kilichokuwa kikiwakilishwa zaidi ya maneno yake. Maneno yake yana nguvu ya kufanya mambo upya, lakini ilikuwa ni kwa jinsi yake ya kuongea. Ni vigumu kuelezea, lakini ni hakika kwamba alivyo ongea, aliwasilisha pia nguvu, utulivu, hali ya kuguswa na kukubali na pia uwepo wake. Aliwakilisha uwepo wake wa Kimungu bila dosari. Watu walitambua tu huyu mtu, Yesu , ni tofauti na wengine wote, na kujikuta wakisikiliza kila neno lake.

Mungu anawasiliana nasi kwa namna hii. Yesu bado anaongea nasi. Tunapaswa tu kuwa wasikivu kwa neno lake. Tunapaswa kuwa wasikivu katika njia ambazo Mungu anaongea nasi katika hali ya wazi kabisa yenye kugusa mioyo yetu, na kwa mamlaka yake. Inaweza kuwa ni kitu mtu anasema, au matendo anayofanya mtu yakatugusa. Inaweza kuwa kitabu nilichosoma, au kitu ambacho nasikia katika maandiko. Katika hali yeyote inavyoweza kuwa, tunapaswa kusikiliza kwani ndipo tunapokutana na Yesu mwenyewe. Kujikita katika kufuata njia ya Mungu ni kujitahidi kutokusikiliza vipingamizi na shutuma unazoweza kupata katika kufuata sauti yake. Sauti yake inapaswa kushinda na kukuvuta katika kufanya yale yote anayopenda uyafanye.

Sala:
Bwana, ninaomba niwe msikivu kwa sauti yako isiyo na dosari na katika mamlaka unayo zungumza. Na ninapo kusikiliza, Bwana mpendwa, nisaidie niitike kwa Imani licha ya vipingamizi vya wengine. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni