Jumatatu. 06 Mei. 2024

Tafakari

Jumatano, Februari 28, 2024

Jumatano, Februari 29, 2024
Juma la 2 la Kwaresima

Yer 18:18-20;
Zab 31:5-6,14-16;
Mt 20:17-28.


JE, TWAWEZA KUKINYWEA KIKOMBE CHA YESU?


Ni rahisi kuwa na nia nzuri, lakini hiyo inatosha? Mama mpendwa anamwambia Yesu aagize kwamba wanawe, mmoja aketi upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto katika Ufalme wake. Lakini, ni vizuri kutambua kwamba hakujua alichokuwa akiomba. Yesu alikuwa akienda Yerusalemu sehemu ambayo atapata utukufu wake kwa njia ya mateso msalabani. Ni katika hali hii Yesu anawauliza Yakobo na Yohane kama wanaweza kunywea kikombe hiki. Walikuwa wamealikwa na Yesu kutolea maisha yao kwa sadaka kwa ajili ya upendo kwa wengine. Walipaswa kuacha woga wote na kusema “NDIO” kwa misalaba yao wakati wakumtumikia Kristo na utume wake.

Kumfuata Yesu sio kitu ambacho tunapaswa kufuata nusu nusu. Kama tunataka kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu, tunapaswa kukinywea kikombe cha damu yake takatifu ndani kabisa katika mioyo yetu na kujazwa na zawadi ili tuweze kujitoa wenyewe hata kufikia kiwango cha kujitoa kabisa sadaka. Tunapaswa kuwa tayari kutokuwa na kitu au kushikilia vitu, hata kama ikiwa ni sadaka kubwa. Tunaitwa wote kuwa wafiadini wa kiroho. Hii ina maana kwamba tunapaswa kujikabidhi wenyewe kwa Kristo na mapenzi yake na hii ina maana kwamba tutakuwa tumekufa wenyewe kutoka katika ubinafsi wetu.

“Je, twaweza kukinywea kikombe ambacho Yesu alikinywea?” je, upendo wako kwa Mungu na jirani waweza kuwa mkamilifu kiasi kwamba unakuwa mfiadini katika maana halisi ya neno lenyewe? Jitambue na sema “Ndio” na kunywa katika kikombe cha damu yake Takatifu na kila siku toa maisha yako kwa sadaka kamili. Unastahili na unaweza!

Sala:
Bwana, ninaomba upendo wangu kwako na kwa wengine uongezeke kiasi kwamba sishikilii kitu kingine nyuma yangu. Ninakuomba zawadi ya damu yako Takatifu iwe nguvu katika safari hii ili niweze kuiga sadaka yako kamili ya upendo. Yesu nakumini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni