Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Jumapili, Julai 24, 2016

Jumapili, 24 Julai, 2016

Dominika ya 17 ya Mwaka C wa Kanisa

Mw 18: 20-32;
Zab138: 1-3, 6-8;
Kol 2: 12-14;
Lk 11: 1-13.


BABA YETU!

Wayahudi walijulikana kwa majitoleo yao kwenye sala. Sala ilielezewa katika nyakati tatu. Marabi walikuwa na sala ya kila tukio. Ilikuwa pia ni utamaduni wa Marabi kuwafundisha watu sala mbali mbali ili waweze kuzitumia katika hali zao na nyakati mbali mbali katika maisha ya kila siku. Wafuasi wa Yesu walimuuliza pia Yesu kuhusu sala. Wakati Yesu alipowapa sala aliwapa sala ya mfuasi tunayoiita Baba yetu au Sala ya Bwana. Kila kipengele kinaweza kusimama chenyewe nakujitosheleza kama kifungu cha sala. Tuangalie utajiri wa sala hii:

Baba
Inaanza kwakumuonesha Mungu kuwa ni "Baba". Hatumuiti Bwana au mkuu au Hakimu. Wala hatumuiti, chanzo cha hekima yote, au Muumbaji Bali tunamuita kwa jina la nafsi, Baba, tusipo lipokea hili kama ukweli halisi, itakuwa vigumu kwetu kumuita Mungu " Baba yetu na sio Baba yangu. Kama tutakavyoona Sala ya Bwana ni zaidi ya sala ya kuomba. Ni sala inayo onesha sisi ninani na sisi nini kwa Mungu na kwa wenzetu.

Jina lako litukuzwe
Kwa Wayahudi jina haikuwa tu kiashiria cha kitambulisho. Wakati Musa akiongea na Mungu katika kichaga kilicho waka moto, alitaka kujua jina la Mungu ili afahamu ni nani. Kwanjia nyingine pia ninani anaweza kumfanya Mungu Mtakatifu au jina lake Takatifu? Utakatifu wake hautegemeani na sisi kwa njia yeyeyote. Tunachoomba sisi ni kwamba sisi tukiri utakatifu wake sio tu kwa maneno pia kwa njia ya maisha yetu.

Ufalme wako ufike.

Ufalme wa Mungu tunaweza kuuelewa kama ulimwengu ambamo kila kitu anachosimamia Mungu kinakuwa na uhalisia kamili katika maisha ya watu kila mahali–ulimwemgu uliojengwa katika ukweli, upendo, huruma, haki, uhuru, utu wa kibinadamu, na amani. Ufalme upo mbali tunashindwa kuona uhalisia huu, na wakulaumiwa ni sisi wenyewe. Kwahiyo tunaposema maneno haya hatuombi tuu msaada wa Mungu bali tunajikumbusha wenyewe katika kushiriki kufanya kazi na Mungu ili kufanya Ufalme huo uwe uhalisia wa kweli.

Utupe leo mkate wetu wa kila siku

Nusu ya pili ya sala tunasali zaidi kwaajili ya mahitaji yetu. Tambua tunaomba kwaajili ya mkate, chakula, chetu cha siku, mahitaji yetu ya kila siku. Je, tunaomba kwaajili hiyo? Au hofu zetu zinatufanya tuombe mpaka cha siku nyingi zijazo? Hata hivyo kwakusali namna hii inaelezea imani yetu juu ya Mungu kutujali sisi. Hakuna sababu ya mashaka na wasiwasi kuhusu wakati ujao katika kumtumainia Mungu.

Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavyo wasamehe waliotukosea

Hapa tunasali kwakuomba toba ya makosa yetu tuliyotenda ila sala yetu ina masharti, ikituunganisha tena na wale walio karibu yetu. Tunaomba Mungu atusamehe kwa Yale tulioenda kinyume na kukosea, kwasababu tumesha wasamahe wale wote ambao tunajisikia wametukosea. Tunaomba kushiriki katika hali nzuri ya sifa ya Mungu– utayari wake wa kusamehe sio tu "saba mara sabini" bali kusamehe bila kikomo.

Usitutie katika Kishawishi

Na hatimaye tunaomba tukingwe na vishawishi vijavyo ambavyo vinaweza kutukumba sisi. Vishawishi hivi na majaribu haya yanaweza kutufanya tuanguke na tushindwe kumfuata yeye.

Pengine tunaweza kukubali kwamba hatuitendei haki sala hii wakati mwingine. Sala hii haituweki tu karibu na Mungu bali inatuweka wamoja na karibu sisi kwa sisi. Tukiwa tunaendelea kusali sala ya Bwana, ingekuwa vizuri na manufaa kama tutaisali taratibu, ombi moja baada ya jingine, na hata kutafakari ili iwe na manufaa kwetu na Mungu atukuzwe.

Sala: Baba yetu uliye Mbinguni jina lako litukuzwe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni