Jumatano. 04 Desemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Februari 07, 2024

Jumatano, Februari 07, 2024

JUMA LA 5 LA MWAKA

1 Fal 10:1-10,
Zab 37:5-6,30-31,39-40
Mk 7: 14-23


NDANI NA NJE!


Kile kinacho mtoka mtu kutoka ndani ndicho kinacho mfanya mtu huyo Mtakatifu! Mara nyingi, tunashugulika sana na vitu vilivyopo nje kuliko vile vya ndani. Tunaogopa sana na kuwa na hofu nyingi wenzetu wanasema nini juu yetu, jinsi ninavyo onekana, na muonekano wangu mbele za watu na ulimwengu. Injili ya leo inaelezea swala la Mafarisayo kuhusu kula chakula kinacho mtia mtu najisi. Lakini Yesu kwa upande mwingine anaongelea kuelekea mioyo yetu. Ni kitu ghani kilichopo mioyoni mwetu? Hiki ndicho kinacho tufanya jinsi tulivyo.

Yesu anataka kutuelekeza kuhusu kushika sheria ya Mungu katika hali ya utakatifu. Anaelezea kuhusu namna ya Mafarisayo kuhusu hofu yao ya jinsi wanavyo onekana mbele ya watu. Muonekano wao wa njee wa jinsi ya kushika sheria inaonekana jinsi ghani walivyo na wasi wasi juu ya jinsi watu wanavyo waona na jinsi wanavyo onekana machoni pao. Wanataka kuonekana watakatifu machoni pao. Lakini huo ni muonekano tuu wa nje sio ukweli halisi. Kwasababu hii Yesu anawasisitizia juu ya mambo ya ndani ya moyo. Hata kama watu hawataona lakini Mungu anaona yote. Kile kilichopo ndani ya mioyo yetu kinaweza kuleta uharibifu mkubwa au kikatujenga sana na kuleta mambo mazuri. Kuna kitu kimoja tu ambacho ni muhimu. Mungu ananifikiria je? Au Mungu ananiona je?

Tutafakari leo, juu ya kile ambacho kipo ndani ya mioyo yetu. Kwanini tunafanya tunacho fanya na kwanini tuna amua kama tulivyo amua? Je, ni uchaguzi unaotoka katika moyo ulio mwaminifu? Au je, ni uchaguzi uliojikita juu ya jinsi nitakavyo onekana? Tujichunguze kama misukumo yetu inatoka katika moyo ambao umejiunga ndani na mwaminifu kama ule wa Kristo.

Sala:
Bwana, fanya misukumo yangu iwe mitakatifu. Nisaidie niweze kutambua kuwa utakatifu unapatikana katika kukutumikia wewe na sio katika kutafuta sifa binafsi na kujitumikia. Ninakupenda Bwana wangu. Yesu, ninakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni