Jumapili. 05 Mei. 2024

Tafakari

Alhamisi, Februari 01, 2024

Februari 1, 2024

JUMA LA 4 LA MWAKA

2 Falm
Nya 29:10-12
Mk 6:7-13


SAFARI ISIYO HITAJI MIZIGO


Tunapo safari mara nyingi katika maisha yetu mara nyingi huwa tunabeba mizigo. Lakini mizigo mara nyingi inatufanya tusiwe wepesi sana katika kuendelea na safari yetu bila usumbufu. Ndio hivyo Yesu anawaonya mitume wake wasibebe mizigo wala kushikamana na vitu katatika safari yao ya utume. Kilicho cha muhimu ni kuwa waminifu kwa Mungu. Kutokufungamana na mali au malimwengu ambayo yatakufanya ushindwe kuhubiri neno lake vizuri.

Ndugu yangu jiulize ni jambo gani linalo kufunga ushindwe kuhubiri neno la Mungu vizuri? Je ni pesa? Au mali? Ni mzigo gani unao chelewesha safari yako ya kumtangaza Yesu? Jiulize na muombe Yesu akusaidie kuutua na kuanza safari Upya kwa maisha ya neema.

Sala:
Bwana nakuomba unisaidie niweze kushika kiaminifu wito huu wa kutangaza neno lako kama Mkristo. Nisaidie nikushuhudie daima.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni