Ijumaa. 23 Februari. 2024

Tafakari

Jumapili, Februari 04, 2024

Jumapili, Februari, 2024,
Dominika ya 5 ya Mwaka wa Kanisa

------------------------------------------------------------------
Somo la 1: Ayubu 7:1-4,6-7
Ayubu analia kwasababu ya mateso yake na maisha yake.

Wimbo wa Katikati: Zab 147:1-6 wimbo wa sifa kwa Mungu kwa sababu ya wema wake kwangu.

Somo la 2:1 Kor 9:16-19,22-23
Paul anaelezea sababu zinamfanya ahubiri Injili na sababu kwanini hatakubali msaada wa kifedha wa Wakorintho.

Injili Mk 1:29-39 Yesu anamponya Mama wa Simoni na wengine wengi pia.
------------------------------------------------------------------

“NA HIVYO NA SASA PIA”

Katika maisha yetu tunaweza kupata taabu na kuishi tukijiuliza maswali yafuatayo. ‘Maisha yangu yanaonekana magumu; yamejazwa machungu, kuchoka na kuhangaikia mahangaiko ya maisha ambayo yamesababishwa na wengine; maisha hayachukuliki. Je, yataisha kweli? Je kuna Mungu anayeona haya yanayotokea?;Waweza kujiuliza kama ni mwema sana kwanini hatusaidii? Tunaumia kwa mawazo, kukata tamaa na mahangaiko mbali mbali? Kwakujibu haya maswali yanahitaji falsafa ndefu na teolojia ndefu.

"Kwanini" Mungu ameweka ndani mwetu imani kubwa? Tunaweza kuwa kwa jinsi tunavyotamani kuwa kama tutafanya kazi pamoja naye, kama tutajiweka sisi katika upendo wake mkubwa na kuruhusu upendo wake uingie ndani mwetu, hili linaweza kutokea tu ndani mwetu na kwa ulimwengu unaotuzunguka na kutupatia changamoto. Kuna nguvu nyingi zinatusukuma ndani mwetu. Tunapigana kama anavyosema Mt. Paulo tunapiga vita vya kiroho, kumwangusha shetani anaye pigana nasi ndani yetu akitaka kutuangusha.

Kuna nyakati ambazo tunapaswa kuweka pembeni maswali ya “kanini? Na kuchukua hatua ni nanmna ghani tunaweza kupigana na yale ambayo yanaharibu Amani yetu badala ya kubaki tukiwa tunafikiria tu maswala ya kanini. Pengine njia ya kutokupeleka sisi Amani nakuhangaika kusaidia kuleta Amani ya wengine na kuwafungua katika vifungo vyao badala ya kubakia kukaa chini na kuanza kufikiria juu ya kukosa kwetu raha. Hili ndilo Mt. Paulo anatualika tulifanye.

Somo la Injili ya leo linaonesha picha nzima ya utume wa Yesu, kuhubiri, kuponya magonjwa, kutoa pepo wabaya, kuwaponya wagonjwa na pili kutofungama na mahali, kuondoka na kuhubiri sehemu nyingine. Injili ya Marko inatuambia kwamba Yesu aliyafanya haya yote katika Galilaya yote.

Ishara ya Yesu kua na huruma na kuwaponya wagonjwa ni ishara ya uwepo wa Ufalme wa Mungu. Kanisa linaendeleza kuunyosha mkono wa uponyaji wa Yesu kwa njia ya sakramenti ya mpako wa wagonjwa. Kwa sakramenti hii Kanisa linasali kwa ajili ya uponyaji wa roho na mwili, msamaha wa dhambi ka njia ya Sakramenti ya kitubio na kuwapa faraja wale wote walio wagonjwa.

Yesu katika somo la Injili pia tunajifunza maisha yake ya sala. Umuhimu wa sala. Kutenga muda kwa ajili ya kuongea na Baba yake kwakweli ameuzingatia sana. Sisi nasi ndugu zangu tunaalikwa kutenga muda kwa ajli ya Mungu. Tumekua waongeaji sana, na wenye kusikiliza mambo mengi yasio ya kuleta baraka na tumesahau kumpa Mungu muda aongee na sisi. Tumethamini sana kazi zetu kuliko hata sala, tumeunganishwa na Tv kutazama movie, katuni,mipira, michezo ya kuigiza lakini ni ajabu kwamba hatujaunganishwa na sala na badala yake Tv imechukua ile sehemu ya kutundukia msalaba na kusali, tunatazama Tv na simu zetu mnoo, kiasi kwamba tumesahau kutenga muda wakuongea na Baba yetu. Tumevutwa na picha mbali mbali tofauti kabisa na picha za Kristo aliyetukomboa, watu tumekua tayari kupamba nyumba zetu kwa picha za wanyama tena wakali kama simba, chui, n’gee, kuchonga hata vinyago na kuweka vyungu vya rangi mbali mbali, ambapo katika uhalisi hakuna aliyekombolewa kwa damu ya wanyama hao wala kukombolewa na ishara nyingine. Tumesahau kuweka zile ishara zetu za ukombozi ambazo ni chapa ya Mwanakondoo (Ufu 14), ambazo ndizo zinatutambulisha Kamba sisi ni wafuasi wa Mwanakondoo wa Mungu. Hivi vyote vimetufanya daima tuwe na mitazamo ya kiulimwengu na katika uhalisia inakuwa ngumu hata kuvuta hisia ya kutaka kukutana na Yesu na kuingia katika faragha na kukutana na Yesu kama Yesu alivyo kutana na Baba yake kwa njia ya sala. Tubadili aina ya maisha tumtangulize Yesu na tujenge mazingira ya kukutana nae, kwa mfano kama wewe unatazama vipicha viovu tu kwenye simu au kwenye Tv, utajenga wapi hata mawazo ya kupenda kukutana na Yesu? Tubadilike.

Tunaweza kukumbwa na magonjwa mbali mbali hata wakati mwingine tukakata tamaa kabisa na kuishi tu kujiuliza kwanini mimi?, daima usisahamu tumaini letu ni Yesu , maswali haya anayajibu yeye mwenywe, usipoteze muda wako kuyafikiria, weka Imani yako kwake yeye anaponya hata yale ambayo kwa macho ya kibinadamu yanaonekana kama hayawezekani tena, yeye atatenda tu. Tuwe jasiri kama Ayubu tumtumainie Mungu kwa njia ya Kristo na hakika atatuponya na kutuondoa katika taabu kama alivyo fanya katika somo la Injili.

Paulo anatusaidia na kutufundhisha kitu cha muhimu sana katika somo la pili, jinsi ya hatari ya mali au kushikamana na fedha kunavyoweza mtu ashindwe kuihubiri Injili ya Yesu kwani watu wanaohitaji kuhubiriwa, wana kiu na neno la Mungu, watu aliokata tamaa tusiache kwenda kuwafariji, kuwasaidia watu na kuwaombea katika magonjwa yao. Yesu mwenyewe awape matumaini ya kweli.

Maoni


Ingia utoe maoni