Jumatatu, Januari 22, 2024
Jumatatu, Januari 22, 2024.
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
2 Sam. 5:1-7,10;
Zab. 89:19-21, 24-25 (K) 24;
Mk 3: 22-30.
KUACHA DHAMBI
Leo sehemu ya Injili inatufunulia kuwa kuna dhambi Fulani, dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ambayo haita samehewa. Hii dhambi ni ipi? Kwanini hai sameheki? Hii ni hali ambayo mtu anatenda dhambi ya mauti na kushindwa kujisikia hali ya kutotubu na kujiona kama hana kosa au kukataa huruma ya Mungu inayo muita kufanya toba ya kweli. Hali hii yakuto jisikia kwamba ametenda dhambi inafunga mlango wakuruhusu huruma ya Mungu. Lakini pia itambulike kwamba, wakati roho ya mtu inapo badilika na kuonyesha kutubu kwasababu ya dhambi, Mungu anamkaribisha mara moja mtu huyo kwa mikono miwili. Mungu hawezi kamwe kumkataa mtu yeyote anaye kwenda kwake kumwomba msamaha kwa moyo mnyofu.
Tutafakari juu ya huruma ya Mungu isio na kikomo, na kutafakari juu ya jukumu letu la kujinyenyekeza mbele za Mungu tunapokosa. Tutimize jukumu letu kwa moyo wa unyofu na Mungu atatupa huruma yake. Hakuna dhambi iliyo kubwa kwa Mungu mtu amwendeapo Mungu kwa moyo mnyofu.
Sala:
Bwana, Yesu Kristo, mwana wa Mungu aliye hai, nihurumie mimi mdhambi. Ninakiri dhambi zangu na ninaomba unisamehe. Nisaidie Bwana wangu, nitazame ndani mwangu na nijisikie huzuni kwa dhambi zangu na kujikabidhi katika huruma yako ya Kimungu. Ninakushukuru kwa upendo wako mkamilifu kwangu na kwa wote. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni