Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Januari 17, 2024

JANUARI 17, 2024
JUMA LA 2 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA MT. ABATE

1Sam. 17:32-33, 37, 40-51
Zab. 144:1-2,9-10 (K) 1
Mk 3: 1-6


DHAMBI INATIA MAWINGU MAISHA YETU!

Haikuchukua muda kwa Mafarisayo wivu juu ya Yesu kutanda fikra zao. Mafarisayo walitaka watu wa waangalie na kuwaheshimu kama walimu waaminifu wa sheria. Hivyo, Yesu alivyojionesha, na watu wakawa wanashangazwa na mamlaka aliokuwa akifundisha nayo, mara moja Mafarisayo walianza kumpinga. Jambo la huzuni ambalo tunaona katika matendo yao, ni kwamba, wanaonekana kuwa vipofu, wivu ukiwajaa na kuwaweka mbali na ukweli kiasi kwamba wanashindwa wanafanya kama watu wasiofikiri. Dhambi inatuchanganya sisi, hasa dhambi za ndani ya roho, kama vile, majivuno, wivu na hasira. Na hivyo, mmoja anavyo chukuliwa na moja ya dhambi hizi, mtu huyo hajitambui ni kwa jinsi ghani uwezo wa kufikiri unavyopungua.

Yesu anawekwa katika hali ambayo anaamua kumponya mtu mmoja wakati wa Sabato. Hili ni tendo la huruma. Linafanywa kwa mapendo ili mtu huyu aweze kutoka katika mateso yake. Ingawaje huu ni muujiza wa pekee, akili za mafarisayo zilizo tibuka wana angalia njia tu ya kubadili kitendo hiki cha huruma kuwa kama kitendo kiovu. Sisi pia tunajitahidi katika hali moja au nyingine, kwa dhambi kama hizi. Mwenzetu anatenda jambo jema, sisi tunajaribu kulibadilisha na kutaka lionekane ni baya, kwa hofu ya kuogopa kupoteza umaarufu wetu. Sisi pia tunajikuta tunaruhusu wivu na hasira kuingia ndani mwetu na kuharibu hali yetu ya kuhusiana na wenzetu. Ni mara nyingi tumejikuta tukihalalisha matendo yetu kama Mafarisayo wanalivyofanya. Tuchunguze maisha yetu na tumwombe Yesu atuponye na kututakasa.


Sala:
Bwana Yesu, nisamehe mimi kwa dhambi zangu. Ninaomba msamaha na ninasali ili niweze kuona yote yanayo funika uwezo wangu wa kufikiri na kutenda. Niweke huru na unisaidie nikupende wewe na jirani zangu kwa upendo mtakatifu ulio niitia. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni