Jumamosi. 04 Mei. 2024

Tafakari

Jumapili, Januari 07, 2024

Januari 7, 2024.
------------------------------------------------

JUMAMOSI, SHEREHE YA EPIFANIA (TOKEO LA BWANA)

Somo la 1: Isa 60:1-6 Nabii Isaya anatoa utabiri wa Yerusalemu yenye furaha na kurudi kutoka kwao utumwani, lakini maono haya yalikuwa yakitabiri ujio wa Kristo ambaye ataunganisha mataifa yote.

Wimbo wa katikati Zab 72:1-2, 7-8, 10-13 Mataifa yote ya ulimwengu yatakuja kukusujudu wewe Bwana. Mbele yako wafalme wote watasujudu na kukutumikia.

Somo 2: Efe 3:2-3, 5-6 Paulo anatoa siri ya utume wake: ametumwa na Mungu kuja kuhubiri habari njema kwa watu wa mataifa yote, watu ambao Mungu amewachaguwa kuwa wake pamoja na Wayahudi.

Injili: Mt 2:1-12 Tunaona Mamajusi watatu wakienda Betlehemu na kumchukulia mtoto Yesu zawadi na kumwabud.
.
------------------------------------------------

KILA GOTI LITAPIGWA KWAKE ( Fil 2:10)!

Katika somo la kwanza, katika ono lake la kinabii, Isaya anaona ujio wa Mungu ulimwenguni. Utakuja muda ambapo watu wote wataletwa pamoja mbele ya Bwana na watabarikiwa sana. Utukufu wa Bwana utashuka ulimwenguni na utukufu wake utauzunguka uumbaji wote. Tukio hili takatifu litalibadilisha jiji la Yerusalemu na wale wote wanaofanya kazi na kuvumilia watapokea mwanga wa uhai.

Katika somo la pili, Paulo anaifumbua siri ambayo Mungu anaitoa kwa utukufu wake watu wote pamoja na wapagani, kuwafanya warithi wa ufalme wake. Anasema “sasa imefunguliwa kuwa wapagani wanashiriki urithi ule ule”. Ukombozi wa ulimwengu, Mungu pia anawapenda wasio Wakristo kwani wao pia ni wapokeaji.

Leo tunasherehekea sherehe ya Tokeo la Bwana. Ni sherehe ya dhihirisho la Bwana wetu kwa watu wa Mataifa. Kulikuwa na mama jusi watatu kutoka mashariki waliokuja kwa Mfalme mpya aliyezaliwa. Mama jusi hawa, watu wa mataifa, ambao hawakuwa katika utajiri wa pamoja wa Waisraeli, walikuwa ni watu waliosoma nyota kwa lengo la kubaini siri na ujumbe wake. Walipokuja katika mahakama ya mfalme, walimuuliza Herode, yuko wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa? Hawakuuliza kama mfalme wa wayahudi amezaliwa? Walikuwa na uhakika kuwa mfalme alikuwa amekwisha zaliwa. Walikuwa tu hawana uhakika wa sehemu yake alipozaliwa, bali juu ya ukweli kwamba amezaliwa walikuwa nao.

Kama tu vile Yeye alivyo jidhihirisha Yeye Mwenyewe kwa wale mama jusi, kila siku Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwetu sisi katika Ekaristi Takatifu. Tunamtukuza Yeye, tunamshukuru na kumfanya yeye afahamike ulimwenguni kote. Basi tujitoe sisi wenyewe kama zawadi na tuunganike naye na kuhubiri: Mungu amejidhihirisha mwenyewe duniani. Yesu anajitoa mwenyewe zawadi kwa dunia nzima.

Sala:
Bwana, niwezeshe niweze kujitoa Mimi mwenyewe kama zawadi kwako.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni