Jumamosi. 04 Mei. 2024

Tafakari

Jumanne, Januari 02, 2024

Januari 2, 2024
------------------------------------------------
JUMANNE, KIPINDI CHA NOELI

Kumbukumbu ya Basili na Greogori Nazianzeni, Maaskofu na Walimu wa Kanisa

Somo la 1: 1Yn 2:22-28 AnayemkataaYesu ni Mpinga Kristo.

Wimbo wa Katikati: Zab 98: 1-4 Mungu amekumbuka ukweli na upendo kwa watu wake.

Injili: Yn 1:19-28 Yohane Mbatizaji, mtangulizi wa Kristo, anatoa ushuhuda kuhusu Yesu.

------------------------------------------------

UBATIZO MAISHA MAPYA YA NEEMA

Tunaweza kukumbuka kuwa kipindi cha Majilio Injili ilitangaza kuhusu ujio wa Yohane katika jangwa , akihubiri na kubatiza na kukutana na Kristo. Tunasoma huhusu yeye mara nyingi katika Injili ya Yohane mwanzoni. Lakini kipindi cha Noeli kinatupeleka mbali zaidi ya matarajio ya majilio. Sehemu ya Injili ya Yohane inaonesha ikisema “yeye alikuwapo kabla yangu” (Yn 1:15). Ubatizo unaongeza kitu kipya “niliona Roho wa Mungu akija juu yake kama njiwa na kukaa juu yake” (Yn 1:32). Anaonekana hata kutabiri kuhusu sadaka ya Yesu “Tazama Mwanakodoo wa Mungu” (Yn 1:36). Marko anaonesha tokeo la Bwana wakati Yohane alivyo mbatiza Yesu. “wewe ni Mwanangu mpendwa niliye pendezwa nawe” (Mk 1:11). Yohane kwa unyenyekevu wake anajiweka kuwa mtu wa nafasi ya pili. Yohane alikuwa ni daraja kati ya Agano la kale na kipindi kipya cha neema ya Kristo, tunayo sheherekea wakati wa Noeli.

Yohane Mbatizaji yupo hai katika kutangaza kwake, anatuita sisi kutubu na kutuambia daima tuandae njia kwa ajili ya Bwana katika maisha yetu. Ujumbe wake upo hai hadi leo kama ulivyokuwa katika miaka 2000 iliyopita. Wakati alivyokuwa akitembea huku duniani alihubiri ili watu wabadilishe mienendo yao na wamrudie Kristo. Aliandaa njia kwa ajili ya Masiha alivyo ingia katika dunia na hivyo kutupatia zawadi ya uzima wa milele. Ubatizo wa Yohane ulikuwa tofauti na ubatizo wa Kristo. Ubatizo wa Yohane ulikuwa ni ishara ya toba Ubatizo wa Yesu “ulikuwa ni kuzaliwa upya.” Ubatizo wa Yohane ulionesha hali ya kutoka katika maisha ya zamani ya dhambi. Ubatizo wa Yesu unaonesha hali ya kupokea hali mpya ya neema. Maisha ya pekee ya kumpokea Yesu. Je maisha yangu nayatengenezaje yafanane na Yesu? .

Tutafakari leo juu ya mwaka uliopoita na mwaka huu mpya. Je, ni vitu gani napaswa kuviacha ili niweze kumkaribisha Yesu? Tumkaribishe Yesu aingie katika maisha yetu mwaka mzima na siku zote.

Sala:
Bwana, umekuja ulimwenguni kwasababu ya upendo kwetu. Umekuja ili uweze kututoa katika shimo la dhambi. Nisaidie niweze kusubiria yote yaliowekwa kwa ajaili ya wokovu wangu. Ninakuomba niweze kusikia sauti ya Yohane Mbatizaji na kunyoosha njia na kuanza maisha ya kutimiza mapenzi yako matakatifu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni