Jumatatu, Disemba 25, 2023
DESEMBA 25, 2023
------------------------------------------------
JUMATATU, OKTAVA YA NOELI
SHEREHE YA KUZALIWA BWANA
------------------------------------------------
Masomo ya usiku
Somo la 1: Isa 9: 1-7 Isaya anatabiri kitu ambacho tunakifahamu tayari: mtoto amezaliwa kati yetu, tumepewa mtoto mwana mume. Jina lake ni Mshauri wa ajabu, Shujaa wa Mungu, Mungu milele milele, mfalme wa Amani. Huyu mkombozi atawaokoa watu kutoka katika giza na ukandamizaji, na kuwawezesha kuishi katika Amani.
Somo la 2: Tit 2:11-14 Mt. Paulo anatupatia jibu sahihi katika maisha yetu ambalo tunapaswa kufuata kwasababu ya Yesu kuzaliwa kwetu.
Injilil: Lk 2: 1-14 tunasikia Luka akionesha jinsi Yesu alivyo zaliwa Betlehem na wachungaji maskini wakimtangaza.
Misa ya alfajiri
Somo la kwanza 1: Isa 62: 11-12 kwa kuzaliwa kwa Kristo, wakristo wanaweza kuonja furaha ya kutoka katika utumwa wa Babeli.
Somo la 2: Tit 3:4-7 sisi wenyewe hatukutoa kitu ili tustahilishwe kuzaliwa kwa Kristo, bali Mungu alimtuma Mwanae kwa njia ya huruma yake.
Injili: Lk 2: 15-20 pamoja na Maria tuanaalikwa kuwa na furaha kuu kwa kuzaliwa kwa Kritsto, ili pamoja na wachungaji, tuweze kumtukuza Mungu na kumsifu.
Misa ya mchana
Somo la 1: Isa 52: 7-10 wimbo huu wa wana wa Israeli baada ya kurudi kutoka katika utumwa wa Babuloni ni wimbo wetu pia kwa kukombolewa. “Bwana amewafariji watu wake, ameikomboa Yerusalem”. Tukichukuliwa na maono haya, Isaya anapaza sauti na kusema “Miisho yote yaUlimwengu imeuona ukombozi wa Mugu wetu”.
Somo la 2: Ebr :1-6 historia ya Mungu na watu wake kwa muda wote huo ilikuwa ni kuwaandaa watu wampokee Mwanae kwa kipindi Fulani. Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anatupa mwanzo wa unabii wa tukio tunalo adhimisha; baada ya kuongea kupitia Manabii, Mungu anaongea nasi tena kwa njia ya Mwanae ambaye kwa njia yake aliuumba ulimwengu”.
Injilil: Yn 1:1-18 huu ni wimbo wa Neno wa Mungu, chanzo cha uzima wote, ambaye kwa kuja kwake kunatufanya sisi tuwe wana wa Mungu. Mwana wa Milele, mwanga wa daima umefanyika mwili ukakaa kwetu na “tumeuona utukufu wake”.
------------------------------------------------
ZAWADI YETU KUU!
Karl Rahner aliandika “Mungu amekuja. Yupo hapa ulimwenguni. Hivyo kila kitu ni tofauti kwa jinsi tunayo tazamia. Muda umebadilishwa kutoka katika umilele na kushuka katika tukio la ukimya, ujasiri wa wazi umefanya tuone lengo husika. Wakati tunapo sema ni “Noeli”. Tunasema kwamba Mungu ameongea na ulimwengu mwishoni, neno ambalo haliwezi kuondolewa kwasababu ni Mungu ametenda, kwasababu ni Mungu mwenyewe ulimwenguni. Na hili lina maana kwamba, anatupenda sisi, sisi pamoja na dunia. Nipo nanyi, mimi ni Maisha wenu. Mimi ni muda wenu”.
Leo kanisa pamoja na viumbe vyote vinafurahi kwasababu vinafanywa upya kwa kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo. “Neno” na kuweko nuru (Mwa 1:3), ambayo ilileta uumbaji sasa inaongelewa tena, kwa njia ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo. Nuru (Yn 1:8), inaangaza sasa katika ulimwengu. Mungu asiye julikana, sasa amejulikana, Baba anajifunua mwenyewe, kwa njia ya Mwanae, Yesu. Neno amefanyika mwili na sasa amekuja kati ya wanadamu. Kuzaliwa kwa Bwana au Noeli ni sherehe ya furaha-Mungu wetu amechukuwa mwili na kuja kukaa kwetu. Noeli haina maana tu ya Mungu kutuonesha upendo bali unyenyekevu wake aliouchukua na sadaka aliofanya kwa ajili yetu. Yesu mwanga wa ulimwengu amezaliwa ili atupeleke kwenye mwanga wa milele. Noeli sio tu kuzaliwa kwa Yesu, bali ni mwanzo wa upendo kati ya Mungu na wanadamnu, kati ya Mungu na sisi.
Somo la Injili ya Yohane halina habari ya kuzaliwa Betelehemu. Badala yake inazunguka katika maada moja “Neno” Logos kwa Kigiriki. Ingawaje hana habari ya kuzaliwa Kristo, hakuna sehemu aliolala Yesu (pangoni), hakuna wachungaji wala hakuna nyota inayo onekana, kuna maana ya ndani katika Injili, ambapo inazamisha ukamilifu wa fumbo la Umwilisho. Leo kuna aina mbili za maneno ambayo yanaelezea fumbo hili: Neno na mwili, Mwanga na giza.
Katika sehemu ya kwanza, Neno na Mwili, Yahane anaonesha fumbo la umwilisho kwa maneno machache-na neno akafanyika mwili. Neno ni Mungu, ambaye ameumba ulimwengu mzima, ambaye ni mkuu kuliko vyote, ambaye alikuwa ni fumbo kubwa sasa amezaliwa kati yetu, amejifanya mtu na amejidhihirisha mwenyewe kwa ubinadamu wote. Na hili linaweza kushangaza kwanini Mungu ameamua kuwa Mwanadamu? Mungu amekuwa Mwanadamu kwasababu anatujali sisi, anatupenda na hivyo anataka kutukomboa sisi. Na hivyo tunavyo tafakari juu ya fumbo hili la Neno akawa mwili, fumbo la Umwilisho ni Muhimu kutambua ‘Ni Kwa jinsi gani Neno alifanyika mwili’ ni ujembe wa Kiroho unaelezea upendo wa Mungu kwa Mwanadamu.
Yohane anawakilisha fumbo la umwilisho kwakusema Yesu ni Mwanga ambao umekuja ulimwengu ili kufukuza giza katika maisha yetu. Tunatambua kwamba dhambi inatia giza akili na roho ya mwanadamu. Inatupofusha na kutufanya tushindwe kutambua ile iliyo kweli na kushindwa kuona mwanga. Lakini pia Yohane anatangaza kwa ujio wa nuru ambayo ni Yesu ambayo inatutia mwanga katika upofu wetu. Tusipo fungua macho yetu tunaweza tusione hata kama mwanga upo. Hivyo hivyo Yesu anatupatia mwanga wa kiroho, lakini tusipo kuwa tayari kufungua macho ya mioyo yetu kwa Yesu, hatutaweza kuona mwanga wa ukombozi wetu.
Noeli ni kipindi ambacho kimejaa mambo mengi sana ya kufurahisha. Mara nyingi kuna zawadi na makutaniko mbali mbali, chakula na muda wa kufurahia. Lakini zaidi Noeli ni kipindi ambacho tunapaswa kurudi nyumba na kuangalia maana halisi ya fumbo hili takatifu. Tunapaswa kuona kwanza Mungu ameingia katika hali yetu ya kibinadamu na kwa njia hiyo yeye anajitambulisha na kila mmoja aliye karibu nasi katika maisha yetu. Mungu anaelewa maisha ya Kibinadamu! Ameyaishi. Pili, tunapaswa kuelewa kwamba, kuzaliwa kwa Masiha wa ulimwengu kumefunulia kila mmoja wetu kwamba anaalikwa kwake. Usiogope kuingia na kumpa Mungu utukufu kwa ujio wake huu Mtakatifu. Mungu awe nasi daima katika furaha ya mioyo yetu, tunapenda neno lake lifanyike Mwili katika maisha yetu na ndani yetu, tunaomba mwanga wake uondoe giza lote katika maisha yetu, tunaomba tukubali zawadi hii ya Yesu na kunufaika nayo tunapo sheherekea Noeli.
Sala:
Mungu Mwenyezi na Baba wa nuru. Neno wako wa Milele alikuja ulimwenguni katika ukimya wa usiku mtakatifu, na sasa kanisa lako linafurahia kwa kuwa karibu nawe. Fungua mioyo yetu na ongeza maono yetu kwa kwako, ili maisha yetu yajazwe na utukufu na Amani yake. Kwa muunganiko wetu na Mungu, tunaomba tuwe kama yeye, yeye ambaye anayaunganisha maisha yetu na yako. Yesu mzaliwa tunakutumaini.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni