Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Disemba 26, 2023

Desemba 26, 2023
JUMANNE, OKTAVA YA NOELI

Sikukuu ya Mt. Stefano, Shahidi wa kwanza

------------------------------------------------
Somo la 1: Mdo 6:8-10, 7:54-59 Mwandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume analinganisha jinsi Stefano, “akijazwa na neema na nguvu, aliyefanya mambo makuu na ishara kati ya watu,” anaonekana kuwakera watu na hivyo akauwawa.

Wimbo wa katikati: Zab 30: 3-4,6,8,16-17 mikononi mwako Ee Bwana naiweka roho yangu. Wewe ni mwamba wangu. Ninaomba mwanga wako umwangazie mtumishi wako. Niokoe kwa mwanga wako.

Injili: Mt. 10:17-22 Yesu anatabiri jinsi wafuasi wake watakavyo onewa na anawaambia wasiwe na wasi wasi. “atakaye vumilia mpaka mwisho ataokoka kifo”.

------------------------------------------------

YESU NI SABABU. NI LENGO LETU

Ni mabadiliko gani ya muda namna hii! Ni jana tu tumesherekea kwa furaha kuzaliwa Bwana na mkombozi wetu na leo tunafanya sikukuu ya shahidi wa kwanza, Stefano. Jana tulivutwa na hali ya mtoto Yesu kulazwa horini na katika hali ya unyenyekevu, na leo tunasimama kama mashahidi kwa damu iliyomwagwa ya shahidi Stefano kwasababu ya kuungama Imani yake kwa ajili ya mtoto huyu tuliye msheherekea jana. Pengine kuna sababu nyingine za kusherehekea sikukuu ya shahidi wa kwanza wa Yesu mara tu ya sherehe ya kuzaliwa Bwana. Sababu ya kwanza inatupa jibu moja kwa moja umuhimu wetu wakumpa maisha yetu huyu mtoto aliyezaliwa Betelehemu. Tunapaswa kumpa kila kitu bila kujibakiza kitu hata ikiwa ni kwa ajili ya kudhulumiwa uhai wetu kwa ajili yake. Inawezekana ikaonekana kama hali ya kuleta hali ya uzuni nakuharibu furaha furaha yetu. Lakini kwa jicho la Imani sikukuu hii inaongeza ladha na maana halisi ya kusherekea sikukuu ya Noeli. Inatukumbusha kwamba kwa kuzaliwa kwa Kristo tunahitaji tumpe kila kitu kutoka kwetu. Tunapaswa kuwa tayari kutoa maisha yetu bila kujibakiza. Kwa kuzaliwa Mwokozi wa ulimwengu tunapaswa kuacha mambo yote na kuamua kumchagua yeye zaidi ya kitu kingine chochote kile., hata zaidi ya maisha yetu. Ina maana kwamba tunapaswa kujitoa sadaka kwa kila kitu kwa ajili ya Yesu, kuishi bila kujibakiza kwa ajli ya mapenzi yake mtakatifu.

“Yesu ni sababu kwa ajili ya sababu” tunasikia mara nyingi. Ni sababu kwa ajili ya maisha, na sababu ya kumpa maisha yetu bila kujibakiza. Tazama leo juu ya jukumu lilowekwa kwako kwasababu ya kuzaliwa kwa huyu mkombozi wetu duniani. Kwa mtazamo wa kidunia hali hii inaweza kuonekana kuwa mbaya na haivutii. Lakini katika mtazamo wa Imani, tunatambua kwamba kwa kuzaliwa kwake ni sababu yetu ya kuingia katika maisha mapya. Tunaitwa kuingia katika maisha ya neema na kujitoa. Jitazame mwenyewe na anagalia sherehe hizi kama mwaliko wako wa kutimiza jukumu lako uliloitiwa na Mungu, na kujitoa bila kujibakiza. Usiogope kujitoa kabisa kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya wengine. Ni sadaka iliyo bora na inafanywa kuwa bora kabisa na huyu mtoto.

Sala:
Bwana, ninaomba kuzaliwa kwako kunifanye mimi nizaliwe katika maisha mapya ya kujitoa bila kujibakiza. Ninaomba unisaidie niweze kuiga upendo wa Mt. Stefano aliokuwa nao kwako niweze kuishi maisha mazuri ya upendo. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni