Alhamisi, Disemba 28, 2023
Desemba 28, 2023
------------------------------------------------
ALHAMISI, OKTAVA YA NOELI, Sikukuu ya Watoto Mashahidi
Somo la 1: 1Yn 1:5 – 2:2 Yohana anatuambia kwamba sisi ni wakosefu tunamuhitaji Kristo. Jitihada yake kubwa ni kutusaidia sisi tuwe mbali na dhambi.
Wimbo wa Katikati: Zab 123:2-5,7-8 Maisha yetu, kama ndege, yameokoka katika mtego wa wawindaji, kwani msaada wetu upo katika jina la Bwana aliyeumba mbingu na nchi.
Injili: Mt 2: 13-18 Mathayo analinganisha kwenda kwa mtoto Yesu Misri na mauaji ya watoto wachanga-watoto wote wa kiumbe wenye umri chini ya miaka miwili. Hawa watoto watakatifu waliuwawa kwasababu ya Kristo. Walimfuata Mwanakondoo asiye na hatia, na kutangaza milele utukufu wa Bwana.
------------------------------------------------
MUNGU ANAWEZA KUFANYA MAMBO YOTE KUWA MAPYA!
Leo tunapewa mashahidi watoto watakatifu, walio uwawa kwasababu ya wivu na chuki ya Herode, kwasababu ya kutaka kumuuwa Yesu na kumuangamiza mfalme ambaye alizaliwa. Tunaweza kufikiria kuhusu kilio kilicho tawala huko Betlehemu wakati watoto hawa walivyokuwa wakiuwawa, mahangaiko ya wazazi wao wakitazama bila msaada, unyama wa maskari. Kwa njia nyingine, inashangaza kwamba Mungu aliruhusu haya. Kwa njia nyingine, kwa upande wa Imani ya ndani, na ya milele na milele, hawa watoto watavaa mavazi meupe na taji la utukufu la mashahidi na wataheshimiwa na malaika na watakatifu wote kwa kuwa mashahidi wa kumshuhudia Mfalme aliyezaliwa. Ingawaje hili pengine lisingeweza kueleweka kwa wakati huo na kuondoa maumivu, hali hii itawafanya familia hizo kujisikia wameingia katika haki ya mbinguni.
Ushahidi wao unatujulisha kwamba kuna wakati mwingine ambapo mambo hayapo katika haki na sawa. Hata tuingie katika mateso ya hali gani, tunapaswa kutambua kwamba Mwana wa Mungu alikuja katika ulimwengu huu, nakuchukuwa hali yetu ya kibinadamu ulio anguka, ili afanye mambo yote sawa. Tuache umwilisho wake, kifoo na ufufuko wake ufanye yote upya na kutupatia taji la mateso yetu. Kama utamruhusu yeye, Bwana atakuwa mshindi katika maisha yako.
Kuuwawa kwa hawa watoto wasio na hatia (wasio weza kuongea) ni moja wapo ya mambo yanayoweza kuonekana kama yanaharibu furaha ya Noeli. Maisha yao yalifupishwa na Mfalme mwenye kupenda madaraka. Matumaini ya wazazi wao yalifungwa. Tunaomba sikukuu hii itukumbushe kuhusu kuheshimu aina zote za maisha na neema ya kumtendea kila mtu kwa utu na heshima. Tunaomba ituletee hali ya kulinda utu na maisha ya mwanadamu, kwa kuwa watu wenye sauti kwa wasio na sauti, wale watoto walio tumboni mwa mama zao.
Sala:
Bwana, hawa watoto wamekuwa kwako kama matunda ya kwanza ya Mwanao, Mwanakondoo popote aendapo. Tunaomba maisha yetu pia yatoe ushuhuda kwa Imani tunayo kiri kwa midomo yetu.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni