Jumatano. 30 Oktoba. 2024

Tafakari

Jumatano, Novemba 01, 2023

Alhamisi, Novemba 2, 2023
Juma la 30 la Mwaka

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU WOTE

Is 29:6-9;
Zab 22;
Rom 5:5-11;
Yn 6:37-40


MIMI NI UFUFUO NA UZIMA!

Leo Kanisa Katoliki linawaombea watoto wake, ambao katika siku ya kufa, japo walitamani utukufu usio na mwisho Mbinguni, hawakuwa wamejiandaa vyema kuingia katika furaha hiyo na pia hawastahili kwenda motoni. Hawa ni roho zilizoko twaharani- ambao wanatakaswa ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni. Lakini pia sisi tujifunze kitu kwamba kila mmoja wetu amesogea siku moja kuelekea kifo. Ni njia yetu wote.

Sala kwa ajli ya marehemu zilianza na Wakristo wa kwanza, mwanzoni kabisa, kuwaombea mashahidi wa kwanza. Walifanya hivyo kumshukuru Mungu Mwenyezi kwa ajili ya mashahidi wa kwanza kwa ujasiri wao, na zaidi sana kwa Imani yao. Walifanya hivyo kwasababu walitambua kifungo kisichoweza kuvunjwa kinacho tuunganisha sisi ndani ya Kristo, walio hao na waliokufa pia. Kifo hakiwezi kuvunja na kutenga familia ya Kristo, hakiwezi kuharibu umoja na muunganiko wetu tunao shiriki katika Kristo sisi zote kama tupo hapa duniani au tumeenda katika maisha yajayo.

Kuwaombea wafu ina msingi wake katika maandiko matakatifu “na hivyo (Yuda Wamakabayo) akafanya maombi kwa ajili ya kuwaombea wale waliokufa, ili wasamehewe dhambi zao” (2 Mak 12:46). Kuanzia mwanzoni, Kanisa limeheshimu kuwakumbuka marehemu na kutolea sala kwa ajili yao, na juu ya yote sadaka ya Ekaristi, ili waoshwe, waweze kupata heri ya mwanga wa Mungu. Kanisa pia linahimiza kutolea sadaka, rehema, na kazi za toba kwa niaba ya marehemu (KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI, 1032).

Lakini hata tungekuwa na ujasiri namna ghani na hata tukipokea ukweli katika hali ya chanya, siku ya kuiacha dunia hii haieleweki na ni lazima, kwasababu kunakuwepo na utengano wa mwili na roho. Hivyo Kanisa linatuhimiza kila mara kujiandaa wenyewe kila mara kwa saa ya kufa kwetu.

Sala:
Mungu mwenye nguvu na huruma, umefanya kifo kiwe mlango wakuingia uzima wa milele. Uwatazame kwa huruma ndugu zetu marehemu, wafanye wawe pamoja na Mwanao kwa mateso na kifo, ili, wakiwa wamefunikwa na damu ya Kristo, waweze kuja mbele zako wakiwa huru kutoka katika dhambi. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni