Jumatano. 06 Desemba. 2023

Tafakari

Jumanne, Oktoba 31, 2023

Jumanne, Oktoba 31, 2023
Juma la 30 la Mwaka

Rom 8: 18-25;
Zab 125: 1-6 (K) 3;
Lk 13: 18-21.


UFALME WA MUNGU NDANI MWETU


Ni ufalme ghani unao hubiriwa na Yesu? Mfano wa punji ya haradali na chachu unaelezea sifa za muhimu za Ufalme wa Mungu alio hubiri Yesu: udogo wake, tabia yake yakutokuonekana kirahisi; kazi yake na uwepo wake.

Yesu leo anafananisha ufalme wa Mungu na punji ya haradali na chachu. Puche ya haradali ni ndogo tena sana. Inapopandwa ardhini inakuwa na kuwa mti mkubwa ambapo ndege wa angani hupata makao. Lakini, pamoja na kwamba ni ndogo, na haijulikani na kujificha inapokuwa ardhini haibaki hapo tu bali huchipua na kumea. Chachu kidogo sana, ambayo huwezi kuiona kwa macho baada ya kuwekwa katika unga, haibaki kama ilivyo bali huumua unga wote.

Tabia ya Uwepo wake na utimilifu wake ujao wa Ufalme wa Mungu unaweza kuwa wetu tu kama matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Ufalme wa Mungu upo hai katika mioyo yetu. Wongofu wa mioyo yetu unachukua muda Fulani au wakati Fulani. Kila siku na kila wakati ni muhimu. Tuna nyakati Fulani ambazo tunaweza kusema kwakweli zilikuwa nyakati za wongofu wetu. Lakini wongovu wa roho ni sawa na chachu kidogo ambayo hufanya matokeo makubwa ya maisha makubwa. Wongofu wa moyo unachukua hatua kwa hatua. Tunamruhusu Roho Mtakatifu aongoze maisha yetu kwa undani zaidi, na kadiri ya siku zinavyoenda sisi tunakuwa katika utakatifu zaidi na zaidi.

Punji, au chachu ni “ukombozi ndani ya Kristo”, ni kule kukutana na Kristo, ambapo kila mwanadamu hutamani na kutumaini. Paulo katika barua yake kwa Warumi ansasema ukombozi ni kitu kisicho onekana (Kama Ufalme wa Mungu), lakini ni kitu ambacho kila kiumbe kinakuwa, au kutumaini. Dunia inayo ipokea mbegu hii au unga unao pokea chachu hii ni sisi wenyewe. Kazi isio onekana kwa macho ni Roho Mtakatifu (rej. Rom 8:23), ambaye anatuweka huru kutoka katika mipaka yetu, na kukuwa bila kipimo. Kama vile mti mkubwa, na maisha yetu yakujikabidhi kwa Yesu yatatufanya sisi kuwa na tumaino kwa Mungu na kujitoa kwa ajili ya wengine kuja kupata pumziko.

Sala.
Bwana Yesu, ninatamani kuwa Mtakatifu. Ninatamani kufanywa upya siku baada ya siku. Nisaidie mimi niweze kubadilika siku baada ya siku katika maisha yangu ili niweze kutembea katika njia ambayo wewe unapenda. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni